WATUMISHI 33 KUTOKA IDARA YA UTAWALA NA IDARA YA AFYA WAPATIWA MAFUNZO YA MFUMO WA MALIPO YA SERIKALI (FFARS)
Wataalamu kutoka kitengo cha fedha kwa kushirikiana na wataalamu wa Tehama wametoa mafunzo ya siku mbili ya mfumo wa malipo ya serikali(FFARS) kwa watendaji wa kata na waganga wafawidhi wa zahanati za kata.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo haya Bw. Godfrey ntembeje ambaye ni muhazini wa halmashauri amesema,”tunawapa mafunzo haya lengo ikiwa ni kuwajengea uwezo ili mfahamu namna ya kutumia mfumo huu wa malipo ya serikali kwani mpaka sasa kwenye kata zenu mlikuwa mkitumia vitabu tunataka tutoke huko hivyo niwaombe msikilize kwa makini ili ikifika muda wa kufanya kazi kusiwepo na mtu yeyote asiyefahamu namna ya kuutumia mfumo huu”.
Aidha mkufunzi wa mafunzo haya bw. Sospeter Marcely ambaye ndiye mkufunzi wa mafunzo haya amesema,”tunawafundisha kwa lengo la kuwajengea uwezo ili waufahamu kwa ukaribu Zaidi mfumo huu wa malipo serikalini(FFARS)ili wanaporudi kwenye maeneo yao ya kutoa huduma waweze kufanya kwa ufanisi Zaidi”.
Kwaupande wao baadhi ya washiriki wa mafunzo haya wamesema wanaishukuru halmashauri kwa kuendelea kutoa fursa mbalimbali za mafunzo wa watumishi wa kada mbalimbali kwani hii inawasaidia kuongeza ufanisi katika utendaji wao wa kazi na kwamba wanakuwa bora kwa kila nafasi watakayopewa kusimulia kwani wanakuwa wanauelewa wa kutoosha mna kuahidi kuutumia ujuzi huu walioupata kuhakikisha wanatoa huduma zilizo bora Zaidi kwenye maeneo yao.