WAUGUZI WA HALMASHAURI WATAKIWA KUGFANYA KAZI KWA WELEDI NA NIDHAMU
Katika kuazimisha siku ya wauguzi duniani leo tarehe 12 mei 2023 wauguzi wote wa halmashauri ya mji wametakiwa kufanya kazi kwa weledi na nidhamu ili kuendelea kuwekw Imani na kuondoa dhana potofu kwa watu wanao wahudumia.
Hayo yalisemwa na Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu dr.Erick Mwijage ambaye ni mfamasia wa mji wa kasulu na kusema,”kuekuwa na dhana potofu za wauguzi japo sio wote kuwaomba kina mama pesa ili wawasaidie wakati wa kujifungua jambo ambalo halileti taswira nzuri kwa kada yetu ya afya hivyo niwaombe mfanye kazi kwa weledi na nidhamu ili kuweka heshima kwa watu tunaowahudumia kwa kuona watu wa afya ni watu wenye upendo na huruma”.
Kwa upande wake mmoja wa wauguzi hao Bi sifa Ezekieli alisema ,”maadhimisho haya kwanza yanatukutanisha na kutuunganisha wauguzi ambao tunafanya kazi kwenye vituo mbalimbali vya afya hapa mjini kasulu na vinatukumbusha kufanya kazi kwa weledi na hata wale wenye kuteleza katika majukumu yao kurudi katika msitari niwaombe tu jamii wawe na Imani na sisi wauguzi wauguzi ili watupenafasi ya kuwahudumia vizuri”.
Katika kuhitimisha maadhimisho hayo ya siku ya wauguzi duniani wauguzi hao walifundishana na kukumbushana namna ya kumsaidia motto kupumua kipindi anapozaliwa ,wakaapa kiapo alichoapa mwanzilishi wa wauguzi duniani mama frolence nightingale na kumalizia kwa kuwatembelea wakina mama wajawazito na waliojifungua kasha kuwapatia zawadi>