WAZAZI NA WALEZI WILAYANI KASULU WAONYWA KUTOFICHA WATOTO KIPINDI CHA ZOEZI LA CHANJO
Wazazi na walezi wilayani Kasulu Mkoani Kigoma wametakiwa kuhakikisha hawafichi watoto wao pindi zoezi la utoaji chanjo ya polio litakapoanza ili kumsaidia mtoto kupata kinga dhidi ya magonjwa hayo.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Isaac Mwakisu wakati wa kikao cha kamati ya afya ya msingi(PHC)chenye lengo la kupanga utekelezaji wa chanjo ya polio kwa watoto chini ya miaka 8 na kusema,”kutokana na Imani potofu za kishirikina na kidini wapo baadhi ya wazazi ambao wamekuwa wakificha watoto wao linapokuja suala la chanjo na kwamba atakaye bainika kuficha mtoto asipatiwe chanjo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake”.
Aidha mratibu wa chanjo halmashauri ya mji bi Happyness Munisi amesema,”halmashauri ya kasulu mji imepokea chanjo dozi 109000ambazo zitatolewa katika vituo 15 vitakavyotoa huduma ya chanjo kwa watoto 86,760 umri chini ya miaka 8 wanatarajiwa kupatiwa chanjo ya polio awamu ya kwanza”.
Kwa upande wake mganga mkuu wa halmashauri ya mji wa kasulu Dr.Peter Janga amesema chanjo hii ya polio imejikita Zaidi kwa watoto licha ya kwamba ugonjwa huu unawapata watu wazima pianawaomba viongozi wa dini na siasa kuwa mabalozi wazuri kwa wananchi ili waweze kuondokana na dhana potofu dhidi ya ugonjwa wa polio na kwamba zoezi hili litafanyika nyumba kwa nyumba na maeneo ya wazi kama stendi za mabasi ,mashambani,sokoni,makanisani na msikitini.
Hata hivyo zoezi lautoaji wa chanjo ya polio kwa watoto wenye umri chini ya miaka 8 awamu ya kwanza inatarajiwa kuanza septemba 21 hadi 24 katika mikoa ya Rukwa,Katavi,Songwe,Mbeya,Kigoma na Kagera.