Wenyeviti wa serikali za mtaa wametakiwa kuhakikisha wa namalizia na kutatua migogoro inayowafikia katika mamlaka zao ikiwa ni njia mojawapo ya kutatua kero za wananchi.
Wameelezwa hayo na Mkurugenzi wa Mji Kasulu Mwl. Vumilia Simbeye wakati akifungua mafunzo ya utendaji kazi kwa wenyeviti wa serikali za mtaa yaliyofanyika Januari 06 katika ukumbi wa Halmashauri.
Mwl. Simbeye ameeleza kuwa migogoro ya ardhi imekua ikitokea sana katika ngazi za mitaa hivyo amewaasa viongozi hao kuwa sauti kwa wananchi ambao wanawatumikia.
Aidha amesisitiza wenyeviti hao kujiepusha na masuala ya rushwa pamoja na matumizi mabaya ya madaraka ili kuhakikisha wananchi wanapata haki na stahiki zao kutoka kwenye mamlaka husika.