IDARA YA ELIMU MSINGI
Halmashauri ya Mji wa Kasulu ina jumla ya shule za Msingi 59 za serikali zenye jumla ya wanafunzi 55,322 kati yao wavulana 27448 na wasichana 27,874. Katika kipindi cha robo ya kwanza, 2017/2018 Idara ya Elimu Msingi imefanya kazi zifuatazo:-
· Kufanya vikao vya Kamati za shule za Mwilamvya na Mwibuye kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 6 vya madarasa na vyoo matundu 12.
· Kufuatilia ujenzi wa madarasa 6 na matundu ya vyoo 12 katika shule za Msingi Mwilamvya na Mwibuye. Kila shule ilipata mradi wa ujenzi wa madarasa 3 na matundu 6 ya vyoo. Hali ya maendeleo ya ujenzi hadi sasa .
· Kutoa mafunzo kwa walimu 118 walimu wakuu 59 na waaratibu elimu kata 15 ya Umahiri wa kuhesabu darasa la I na II moduli ya 5-9
· Kufanya marekebisho ya taarifa za TSM na TSA kila kwenye mfumo BEMIS.
· Kuendelea kutoa huduma za kitaaluma na kitaalamu kwa wateja mbalimbali wanaofika ofisini.
· Kuendelea kusimamia utekelezaji wa sera ya ‘’ELIMU BURE’’ kwa wanafunzi wote wa Elimu ya msingi.
· Kusimamia na kufuatailia usafi katika kituo cha Elimu maalum Kabanga.
· Kufanya maandalizi ya mwisho ya Mtihani wa Taifa wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) 2017 pamoja na kufanyika kwa mtihani huo. Maandalizi yaliyofanyika ni pamoja na:-
- Kuandaa vikao vya kamati ya Uendeshaji Mitihani ngazi ya wilaya na Mkoa.
- Kugawa baadhi ya vifaa muhimu kama vile vibao, rubber band na CAL.
- Kufanya uteuzi wa wasimamizi wa Mtihani na kuwasilisha mkoani.
- Kuchukua mtihani wa Taifa wa Kumaliza Elimu ya Msingi kutoka Mkoani kuja Halmashauri..
- Kuandaa bajeti ya Mtihani.
- Kuandaa malipo kwa wasimamizi.
- Kufanya semina ya maelekezi kwa wasimamizi.
- Kutawanya mitihani na wasimamizi katika vituo vya mitihani n.k.
· Kufanyika kwa Mtihani wa Taifa wa Kumakiza Elimu ya Msingi tarehe 06 – 07/09/2017.Taarifa ya watahiniwa ilikuwa kama ifuatavyo:-
WALIOSAJILIWA |
WALIOFANYA MTIHANI |
% |
WASIOFANYA MTIHANI |
% |
||||||
WAV |
WAS |
JML |
WAV |
WAS |
JML |
WAV |
WAS |
JML |
||
1950
|
2293
|
4243
|
1942
|
2280
|
4222
|
99.5
|
8
|
13
|
21
|
0.5
|
· Kuhakiki watumishi hewa. Ni zoezi linalofanyika kila mwezi kwa kutumia Pay roll.
· Kukusanya madai mbalimbali ya watumishi walimu yasiyo mishahara.
· Kuendesha mafunzo kwa Walimu wakuu, walimu wa miradi shuleni wajumbe mmoja moja wa kamati za shule na Mfanyabiashara mmoja mmoja kutoka kila Mtaa. Mafunzo hayo yaliendeshwa na kuwezeshwa na Eguip-Tanzania.
· Kuhudhuria semina ya ugawaji wa vyandarua kwa wanafunzi wa darasa la I -III Mkoa wa Kigoma.
· Kuhamisha na kupokea wanafunzi wanaohama ndani na nje ya Halmashauri.
· Kukusanya takwimu za Walimu kwa majina yao toka kila shule. Zoezi hili lilifanyika hadi Agosti, 2017.
· Kutembelea shule ili kuona hali ya ufundishaji inavyoendelea Shule za Juhudi, Mwenge, Mwilamvya, Nyarumanga, Kanazi na Nyakabondo zimetembelewa.
· Kutembelea shule za Kiganamo, Bogwe, Kalema, Uhuru, Murubona na Umoja ili kuona hali ya utekelezaji wa Mtaala mpya ulioboreshwa.
· Kuhudhuria semina ya Early Grade Mathematics (EGM) iliyoyanyika Kigoma kuanzia Tarehe 1 – 5 /8/2017.
· Kufanya ukaguzi na ufuatiliaji wa huduma za maji, Elimu Afya na usafi wa Mazingira shuleni kwa shule 88 za Msingi na sekondari.
IDARA YA ELIMU SEKONDARI
Idara ya Elimu Sekondari inasimamia shughuli za maendeleo katika Shule 25 za Sekondari, kati ya shule hizo, 11 ni za Serikali na 14 ni shule zisizo za serikali. Idara ina jumla ya walimu 299, Fundi sanifu Maabara 1 na maafisa 4. Idara imetekeleza majukumu yake kwa kipindi cha mwezi April – June, 2017 kwa kuzingatia Mpango Kazi wa Idara 2017/2018 kama ifuatavyo;
2. SHUGHULI NILIZOTEKELEZA
2.1 KUSHIRIKI UENDESHAJI NA USIMAMIZI WA MTIHANI YA KUHITIMU ELIMU YA MSINGI
Idara ya elimu sekondari ilishiriki kikamilifu katika usimamizi na uendeshaji wa Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi PSLE 2017.
2.2 UHAKIKI MADENI YA WALIMU
Idara kwa kushirikiana na timu ya uhakiki wa madeni ya wilaya ilihakiki madeni ya walimu yasiyokuwa ya mishahara kuanzia julai 2016 hadi Juni 2017 na kuyawasilisha mamlaka za juu Mkoa na Wizara.
2.3 KUKUSANYA NA KUJAZA TAKWIMU MBALIMBALI ZA ELIMU KUTOKA SHULENI NA KUZIWASILISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA
Idara ilikusanya takwimu mabalimbali katika shule za sekondari na kuandaa taarifa mbalimbali kulingana na maelekezo na kuziwasilisha katika mamlaka husika
2.4 KUFANYA MAANDALIZI YA MTIHANI WA KIDATO CHA PILI NA CHA NNE MWAKA 2017
Idara imefanya maandalizi ya ufanyikaji wa mitihani ya kidato cha Pili (FTNA), Nne na Maarifa (CSEE & QT), 2017. Mitihani hii inatarajiwa kuanza kufanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba na Novemba 2017.
2.5 KUSIMAMIA UENDESHAJI WA MTIHANI YA UTIMILIFU WA KIDATO CHA NNE (MOCK ) MKOA, NA PRE NATIONAL, 2017
Idara iliratibu maandalizi na ufanyikaji wa mitihani tajwa hapo juu yaani uandaaji wa bajeti, uteuzi wa walimu wa kutunga, kuhakiki, usimamizi wa ufanyikaji, usahihishaji na utoaji wa matokeo ya mtihani na matokeo yalikuwa kama kiambatisho kinavyoonesha. Mtihani wa Pre-National ulifanyika ili kuongeza mazoezi kwa watahiniwa wa shule za serikali na kuwa tayari katika ushindani kwa kufanya mitihani ambayo haikutungwa na walimu wanaofundisha masomo yao.
2.6 KUSIMAMIA UUNDWAJI WA ZA BODI ZA SHULE
Idara ilitoa maelekezo ya namna ya kupendekeza wajumbe wa Bodi za shule kwa shule zote za serikali na zisizo za serikali ambazo Bodi zao ziliisha muda wake ama zilikuwa hazina Bodi na kuhakikisha mapendekezo yote yamepelekwa katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Kigoma.
2.7 KUFANYA UFUATILIJI WA USIMAMIZI WA UFUNDISHAJI NA UJIFUNZAJI
KATIKA SHULE ZA SEKONDARI
Kufanya ufuatiliaji wa ufundishaji na ujifunzaji katika shule za sekondari na kutoa ushauri.
2.8 UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI KATIKA SHULE YA KIGOMA GRAND
Idara ilishiriki taratibu zote za maandalizi katika uwekaji wa jiwe la msingi katika shule ya KIGOMA GRAND tarehe 19 august, 2017. Jiwe la msingi liliwekwa na Mhe.Prof. Joyce Ndalichako (MB), Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia.
2.9 KUENDESHA VIKAO MBALIMBALI VYA KIUTENDAJI
Idara iliendesha vikao kwa ajili ya uboreshaji wa utekelezaji wa majukumu ya kutoa elimu ya sekondari kwa wakuu wa shule za serikali na zisizo za serikali. Vikao hivyo ni kikao cha mrejesho wa
2.10 Kuhudhuria vikao vya Bodi za shule na kutoa ushauri wa changamoto mbalimbali
3.0 MAPOKEZI YA FEDHA
Idara ya Elimu Sekondari katika kipindi cha Robo ya Kwanza ya Julai– Septemba 2017/2018 Imepokea fedha Tsh. 73,201,775.09 na kutekeleza shughuli mbalimbali kwa mchanganuo ufuatao katika jedwali;
Na.
|
MUDA WA KAZI
|
SHUGHULI ILIYOFANYIKA
|
PESA ILIYOPOKELEWA
|
1.
|
Julai
|
Mgawo wa Elimu Bure
|
36,600,357.09
|
2
|
Augost
|
Mgawo wa Fedha za elimu bila malipo
|
36,601,424
|
3
|
Septemba
|
|
73,201,775.09
|
IDARA YA MAENDELEO YA JAMII
Taarifa ya idara ya maendeleo ya jamii ya robo ya kwanza. Katika taarifa hii imegawanyika katika sehemu zifuatazo; Taarifa ya uhakiki wa asasi zisizo za kiserikali (NGOs) ,Taarifa ya mfuko wa wanawake (WDF), na Taarifa ya vikundi vilivyosajiliwa.
Kwa mwaka wa fedha 2017/2018 katika robo ya kwanza, Halmashauri ya Mji wa Kasulu imefanikiwa kisajili vikundi 25 vya wanawake na vijana. Vikundi hivi vinajishughulisha na shughuli mbalimbali za uzalishaji mali kama vilivyoorodheshwa hapa chini:
Na
|
JINA LA KIKUNDI
|
NAMBA YA USAJILI
|
MAHALI KILIPO
|
TAREHE YA USAJILI
|
SHUGHULI ZA KIKUNDI
|
1
|
Chama cha madereva mchomoko
|
KTC /CBO/0099
|
MURUBONA
|
16.07.2015
|
Kusafirisha abiria ndani na nje ya mji wa kasulu
|
2
|
AMANI WOMEN
|
KTC /CBO/0103
|
KUMSENGA
|
22.07.2017
|
Kununua na kuuza mazao
|
3
|
NIYOKURU WAJANE WOMEN GROUP
|
KTC /CBO/0104
|
NYANSHA
|
30.7.2017
|
Kununua na kuuza mazao ya chakula
pamoja na kilimo cha bustani.
|
4
|
KILOMBERO YOUTH GROUP
|
KTC /CBO/0106
|
MURUSI
|
12.8.2017
|
Kupakia mizigo ya mazao ya tumbaku
|
5
|
ILAKOZE GROUP WANAWAKE
|
KTC /CBO/0105
|
MURUSI
|
12.8.2017
|
Mazao ya chakula
|
6
|
TUPENDANE KWA SHAYO WANAWAKE
|
KTC /CBO/0107
|
MURUSI
|
16.8.2017
|
Kuweka na kukopa, kusaidiana katika shida na raha
|
7
|
NNUUR-ISLAMIC WOMEN GROUP
|
KTC /CBO/0109
|
MWILAVYA
|
16.8.2017
|
Kuweka na kukopa
|
8
|
KASULU TUMAINI HISA GROUP
|
KTC /CBO/0111
|
KUMSENGA
|
17.8.2017
|
Kuweka na kukopa
|
9
|
KASULU NEEMA GROUP
|
KTC /CBO/0110
|
KUMSENGA
|
17.8.2017
|
Kuweka na kukopa
|
10
|
TWENDE NA WAKATI WANAWAKE
|
KTC /CBO/0108
|
MURUFITI
|
21.8. 2017
|
Kutoa elimu ya ujasiliamali
|
11
|
JITEGEMEE VIKOBA
|
KTC /CBO/0112
|
HERU-JUU
|
19.8.2017
|
Kuweka na kukopa
|
12
|
UPATANISHO VIJANA GROUP
|
KTC /CBO/0113
|
MURUSI
|
21.8.2017
|
Uuzaji na ununuzi wa mazao
|
13
|
FURAHA WOMEN
|
KTC /CBO/0114
|
MURUSI
|
21.9.2017
|
Uuzaji wa duka la dawa muhimu
|
14
|
TUINUANE WALEMAVU GROUP
|
KTC /CBO/0115
|
NYANSHA
|
11.9.2017
|
Ufugaji wa nguruwe
|
15
|
KILIMO KWANZA WANAWAKE
|
KTC /CBO/0116
|
MURUSI
|
11.9.2017
|
Kilimo cha mihogo
|
16
|
EFSA WOMEN GROUP
|
KTC /CBO/0117
|
MURUSI
|
11.9.2017
|
Uuzaji wa chakula hotel
|
17
|
TUMAINI NYAKALELA
|
KTC /CBO/0118
|
HERU-JUU
|
11.9.2017
|
Ufugaji wa kuku wa kienyeji ujasiliamali kilimo cha mazao ya chakula
|
18
|
EDENI WOMEN GROUP
|
KTC /CBO/0120
|
MURUSI
|
11.9.2017
|
Ununuzi na uuzaji wa mazao
|
19
|
COMPLEX ACT YOUTH GROUP
|
KTC/CBO/0121
|
MURUSI
|
11.09.2017
|
Sanaa ya uingizaji ,ufugaji wa kuku wa mayai
|
20
|
SAYUNI WOMEN GROUP
|
KTC/CBO/0122
|
MURUSI
|
11.09.2017
|
Kuuza na kununua mazao ya chakula
|
21
|
ZANTEL YOUTH GROUP
|
KTC/CBO/0123
|
NYUMBIGWA
|
12.09.2017
|
Kilimo cha matunda
|
22
|
MAANDARIO WOMEN
|
KTC/CBO/0124
|
MURUSI
|
26.29. 2017
|
Kuuza na kununua mazao ya chakula.
|
23
|
VIJANA WAFUGA BATA
|
KTC/CBO/0125
|
MWILAVYA
|
28.09.2017
|
Ufugaji bata.
|
24
|
JITIHADA WOMEN GROUP
|
KTC/CBO/0126
|
KUMSENGA
|
14.03.2017
|
Kuweka na kukopa na kilimo cha chakulaovyamaji.
|
25
|
SHALOOM WOMEN GROUP
|
KTC/CBO/0127
|
MURUSI
|
29.09.2017
|
Uuzaji wa mbegu na mboleafirishaabirianamizigoyao.
|
MASHIRIKA YA SIYO KUWA YA KISERIKALI (NGOs) YALIYO HAKIKIWA NAKUTAMBULIWA KUFANYAKAZI KATIKA HALMASHAURI YA MJI WA KASULU .
Katika Halmashauri ya mji wa Kasulu kuna mashirika 15 yasiyo ya kiserikali (NGOs) yanayotambuliwa na Idara ya Maendeleo ya Jamii. Mashirika haya yanatoa huduma zake ndani na nje ya mipaka ya Halmashauri ya mji wa Kasulu. Baadhi ya mashirika haya yanatoa huduma zake kwa wakimbizi. Aidha mashirika yanayotolewa taarifa zake ni yale ambayo walileta utambulisho na yamekuwa yakileta taarifa zao za utekelezaji. Mashirika hayo yameorodheshwa hapa chini.
TAARIFA YA NGOs ZINAZOFANYAKAZI KATIKA HALMASHAURI YA MJI.
N/S
|
JINA LA NGOs
|
MAHALI ILIPO/ENEO LA OFISI
|
KAZI /SHUGHILI ZA NGOs
|
NAMBA ZA NGOs
|
MWAKA WA WAKUANZA
|
1
|
WESTERN TANGANYIKA ENTERPRENEUR IN AGRICULTUREBAND FISH CAPTIVITY ORGANIZATION (WETAAIFICO)
|
MKOA WA KIGOMA , WILAYA YA KASULU, MTAA WA MRUSI
|
KUJENGA UJUZI WA VITENDO KATIKA KILIMO , UFUGAJI WA WANYAMA NA SAMAKI. UFUGAJI WA NYUKI NA USINDIKAJI WA CHAKULA (NK)
|
OONGOs/00004592
|
15/07/2010
|
2
|
CONSORTIUM
|
KASULU TC MURUSI
|
KUTUNZA MAZINGIRA ,KUWAPATIA ELIMU YA KIAFYA KWA JAMII
|
No S. A 17243
|
24TH JANUARY, 2011
|
3
|
SAVE FOR DEVELOPMENT AND RELIEF ASSOCIATION(SADERA)
|
KASULU TC KIGANAMO
|
KUTOA ELIMU YA AFYA KWA JAMII YA KASULU MJINI NA VIJIJINI. KU WEZESHA VIKUNDI VYA WA NAWAKE NA VIJANA WA KIKE NA KIUME KIUCHUMI.
|
00NGOs/ 00001461
|
12/03/2012
|
4
|
TREECOVER FOUNDATION (TCF)
|
KASULU TC BARABARA YA KIBONDO MKABARA NA OFISI YA HALMASHAUR YA MJI.
|
UTUNZAJI WA MAZINGIRA PAMOJA NA KUANDAA VITARU VYA MITI.
|
OONGOs/ 0009245
|
29TH MAY 2017
|
5
|
WAKWANZA PARALEGAL ORGANIZATION (WAPAO)
|
KASULU TC MURUSI
|
KUELIMISHA JAMII JUU YA MASUALA KISHERIA NA HAKI ZA KIJAMII PAMOJA NA KUSURUHISHA MIGOGORO YA KIJAMII.
|
06/NGOs/08451.
|
|
6
|
HAKI ORGANIZATION
|
KASULU TC MTAA WAMISSION AGRICANA
|
KUTOA HUDUMA ZA KISHERIA KWA WTOTO WA MITAANI , MITAA, WAJANE NA MAYATIMA.
|
SO. NO. 11963
|
11TH AUGUST 2003
|
7
|
TANZANIA AGRICULTURE AND ENVIROMENT DEVELOPMENT ORGANIZATION, (T,A.E.D.O)
|
KASULU T.C MRUVUMU
|
KUTUNZA MAZINGIRA,KUOTESHAJI WA MITI NA UPANDAJI MITI PAMOJA NA KILIMO CHA MSETO KWA KUTUMIA MITI INAYORUTUBISHA ARTHI NA MBOLEA YA SAMADI NA MBOJI
|
SO.14983.
|
2 AUGUST2004
|
8
|
TANZANIA RURAL DEVELOPMENT AND RELIEF ORGANIZATION (TARUDEREO)
|
KASULU TC
T.T.C
|
KUTOA HUDUMA KUSAIDIA WANAWAKE NA VIJANA PAMOJA NA WAKIMBIZI WALIO ATHIRIKA KIJAMII HASA WALE WA LIO MAKAMBINI
|
SO NO 11470
|
|
9
|
FIGHTERS FOR DEVELOPMENT SUSTAINABILITY (FIDESU)
|
|
UTUNZAJI WA MAZINGIRA ,UOTESHAJI WA MICHE YA MITI, AFYA , KILIMO, UFUGAJI WA NYUKI , UFUGAJI WA SAMAKI,KUKU, NA KILIMO CHA MIWA NA MIHOGO.
|
OONGOs/08593
|
16TH MAY 2016
|
10
|
KASULU MOBILE EYE CARE FOUNDATION(KAMECAF)
|
KASULU T.C
KWIZERA
|
KUELIMISHA JAMII KUHUSU MAGONJWA YA MACHO NA KUTOA MATIBABU YAKE.
|
00NGO/0008800
|
25TH OCTOBER/2016
|
11
|
DISABILITY RELIEF SERVICES (DRS)- TANZANIA
|
KASULU TC MATAA WA KWIZERA
|
KUTOA HUDUMU ZA VIWEZESHA (SUPPORTING GEAR) KWA WATU WENYE ULEMAVU KASULU MJINI NA VIJIJINI ILI KUWALAHISHIA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YAO YA KIMAISHA. KUWAJENGEA
|
|
January 2016
|
12
|
BENEVOLENT INSTITUTE OF DEVELOPMENT INITIATIVE IN TANZANIA,(BIDII-TANZANIA)
|
KASULU T.C MTAA WA NYASHA
|
KUTOA MAFUNZO KWA WAKULIMA NA JUU YA MIFUNGO,KUHUSU UFUNGAJI BORA WA NGOMBE WA MAZIWA NA NYAMA YA NGURUWE,MBUZI NA KUKU , NA PAMOJA NA KILIMO BORA CHA MAZAO YA CHAKULA ,
|
SO. 12676
|
AUGUST 2004
|
13
|
KASULU HEALTH HOME BASED CARE ORGANIZATION (KAHHOBACO)
|
KASULU T.C
MTAA WA NYASHA
|
CLINIC YA AFYAYA UZAZI NA MTOTO PAMOJA NA KUTOA ELIMU YA JAMII JUU YA KUZUIA MAGONJWA MBALI MBALI KAMA VILE MALARIA NA HIV/AIDS
|
OO NGO/ 00003052
|
08TH APRIL 2009
|
14
|
TANZANIA HELP ELDERLY AND SINGLE PARENT ORGANIZATION (THESPO)
|
KASULU T.C
JIRANI NA KANISA KUU LA ANGLICANA
|
KUSAIDIA WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA HATARISHI PAMOJA NA KUSAIDIA YATIMA , WAJANE NA WAZEE. KUTOA ELIMU KWA JAMII KUHUSIANA NA MAGONJWA MBALI MBALI IKIWEMO MAGONJWA YA MLIPUKO PAMOJA NA MAZINGIRA.
|
00NGO/00007863
|
5TH MARCH 2015
|
15
|
SAIDIA WAZEE (SAWATA)
|
KASULU T.C
UJENZI
|
KUTOA HUDUMA ZA KUSAIDIA WAZEE KWA AJILI YA KUINUA MAISHA YAO NA KUPUNG O MISONGO YA WAZEENI
|
SO.NO .8039
|
16/10/2008
|
16
|
AMENITY NON PROFIT CHARITY ORGANIZATION (ANCO)
|
KASULU T.C
MURUBONA MTAA WA UMOJA
|
UWEZESHAJI WANAWAKE KIJAMII NA KIUCHUMI PAMOJA NA ILINZI WA HAKI NA USTAWI WA WATOTO
|
O6NGO/00005896
|
19TH OCTOBER 2012
|
MAPENDEKEZO YA VIKUNDI VINAVYOTEGEMEWA KUPATA MIKOPO
s/n
|
Jina la kikundi
|
Kata
|
kiasi
|
Mradi wa kikundi
|
1.
|
Bwiza women
|
Murusi
|
2,000,000
|
Ufugaji wa kuku
|
2.
|
Tupendane women
|
Murusi
|
2,000,000
|
Uuzaji wa mazao
|
3.
|
Tuinuane walemavu group
|
Nyansha
|
2,500,000
|
Ufugaji wa nguruwe
|
4.
|
Tuhudumiane wajane
|
Nyansha
|
3,000,000
|
Kilimo cha bustani ,kuweka na kukopa
|
5
|
Itangigomba women
|
Kumsenga
|
3,000,000
|
Ununuzi na uuzaji wa mazao
|
6
|
Furaha women
|
Murusi
|
3,000,000
|
Duka la dawa baridi
|
7
|
Kayore youth
|
Murubona
|
3,000,000
|
Mradi wa kutengeneza viatu
|
8
|
Mshikamano women
|
Murubona
|
4,000,000
|
Kutengeneza sabuni za maji na masweta
|
9
|
Amani women
|
Kumsenga
|
2,000,000
|
Kulangua mazao na kuuza
|
10
|
Niyonkuru wajane
|
Murubona
|
2,500,000
|
Kununua na kuuza mazao
|
|
Jumla
|
|
27,000,000
|
|
IDARA YA KILIMO NA UMWAGILIAJI
Idara ya Kilimo Umwagiliaji na Ushirika Mji ina jumla ya watumishi 12,kati ya hao watumishi 2 wako ngazi ya ofisi kuu na 10 ngazi ya kata na mtaa.Katika kipindi cha robo ya kwanza cha mwaka wa fedha 2017/18 katika kipindi hiki idara ilitekeleza shughuli kusimamia na kufuatilia ujenzi wa soko la sofya .paomoja na shughuli za ugani kama zilivyoainishwa hapa chini.
HALI YA HEWA.
Katika Kipindi cha robo ya kwanza kimekuwa cha kiangazi ambacho wakulima walikitumia kuzalisha mazao ya bustani hasa mboga za majani ,mahindi na maharage maeneo ya bondeni yenye ardhi oevu.
PEMBEJEO ZA KILIMO
Mwaka huu wa fedha 2017/18 serikali haitatoa ruzuku za pembejeo kwa mfumo wa vocha kama ilivyofanyika kwa miaka ya nyuma badala yake serikali imeelekeza wakala wa pembejeo kutoa bei elekezi kwa mbolea ya kupandia aina ya DAP kuwa itauzwa kwa sh.56,000 badala ya sh 65,000 inayouzwa na wafanyabiashara katika Halmashauri ya Mji wa Kasulu na Urea Kuuzwa kwa sh 43,679 badala y ash.48,000 iliyopo madukani sasa.
4.SHUGHULI ZA UGANI.
Katika msimu wa Kilimo 2017/18 idara ya kilimo imepanga kutekeleza shughuliza
Kwa kuzingatia malengo yafuatayo:-
MALENGO YA KILIMO MSIMU 2017/18
ZAO
|
LENGO(HEKTA)
|
UVUNAJI
TANI
|
MAHINDI
|
30,000
|
52,500
|
JUMLA NDOGO
|
30,000
|
52,500
|
MAHARAGE
|
5950
|
29,750
|
MBAAZI
|
105
|
105
|
NJEGERE
|
12.5
|
12.5
|
JUMLA NDOGO
|
6067.5
|
2,929
|
MIHOGO
|
8960
|
89,600
|
VIAZI VITAMU
|
399
|
3,192
|
VIAZI MVIRINGO
|
70
|
595
|
MAGIMBI
|
18
|
180
|
JUMLA NDOGO
|
9,447
|
93,567
|
VITUNGUU SAUMU
|
10
|
75
|
TANGAWIZI
|
9
|
90
|
JUMLA NDOGO
|
19
|
165
|
NYANYA
|
90
|
2250
|
VITUNGUU
|
62
|
465
|
HOHO
|
28
|
28
|
KABICHI
|
38
|
760
|
MCHICHA
|
21
|
21
|
CHINESE KABICHI
|
7
|
7
|
KAROTI
|
5
|
20
|
NYANYA CHUNGU
|
14
|
72
|
MATANGO
|
6
|
24
|
TIKITI
|
8
|
80
|
JUMLA NDOGO
|
269
|
3,727
|
KAHAWA
|
20
|
13
|
ALIZETI
|
35
|
-
|
KARANGA
|
95
|
95
|
NDIZI MBIVU
|
37
|
225
|
NDIZI MBICHICHI
|
98
|
450
|
MIWA
|
59
|
590
|
JUMLA
|
361
|
1,360
|
MALIMAO
|
12
|
12
|
MACHUNGWA
|
16
|
32
|
CHENZA
|
6
|
12
|
AVOCARDO
|
5
|
50
|
PAPAI
|
12
|
120
|
PASHENI
|
5
|
5
|
JUMLA NDOGO
|
56
|
231
|
JUMLA KUU
|
46,219
|
154,479
|
IDARA YA MAJI
TAARIFA YA UTEKELEZAJI YA IDARA YA MAJI KWA ROBO YA KWANZA
Katika Robo hii ya kwanza Idara ya Maji iliendelea kusimamia ujenzi wa miradi ya maji Kimobwa,Heru juu na Muhunga. Utekelezaji wa miradi hiyo ipo katika hatua mbalimbali ambapo mradi wa maji Heru juu umekamilika kwa 75%, Mradi wa Maji kimobwa umekamilika kwa 79% na Mradi wa maji Muhunga umekamilika kwa 70%. Wakazi katika miradi ya maeneo yote matatu wameanza kunufaika na huduma ya maji kupitia miradi hiyo.Hata hivyo miradi hiyo ilitarajia kukamilika tarehe 09/11/2017 kama fedha ingekuja kwa wakati.Mpaka kufikia hatua hiyo mkandarasi alikuwa amelipwa asilimia 15 ya fedha zote za utekelezaji wa mradi.Mkandarasi katika miradi ya Heru-Juu na Kimobwa ameomba kuongezewa muda wa mwezi mmoja kwani fedha ya miradi hiyo imengia tarehe 02.11.2017 na mkandarasi wa mradi wa muhunga ameomba kuongezewa miezi 2 kwasababu anatakiwa kujenga tenki la Maji ambalo litatakiwa kukaa na maji kwa siku 21 kabla ya kufunikwa.
Vilevile katika Robo hii Idara ya Maji iliendeleza zoezi la kuunda na kusajili vyombo vya Watumia maji. Vyombo vya watumia Maji vimeundwa katika maeneo ya Kanazi, Ruhita, Heru juu, Mwanga B, Nyumbigwa, Kabanga na Msambara. Utaratibu wa kuvisajili umekamilika kwa maeneo ya kabanga na Msambara. Usajili kwa maeneo yaliyobakia umekamilishwa katika Robo ya pili ya mwaka 2017/18.
Changamoto kubwa zinazokabili Idara ya maji hivi sasa ni uzalishaji wa maji mdogo kuliko mahitaji ya maji kwa Wakazi wa Halmashauri ya mji wa Kasulu. Wakazi wanaopata huduma ya maji ni 58%. Katika kukabiliana na Changamoto hili, Mipango ya utekelezaji wa Miradi umeandaliwa na utekelezaji wake umepangwa kufanyika kwa kipindi cha miaka mitano kati ya 2016 -2021. Ujenzi wa miradi ya maji inayoendelea katika maeneo ya kimobwa, Heru juu na Muhunga ni sehemu ya utekelezaji wa mpango hiyo.
Changamoto ingine ni Uhaba wa Watumishi katika sekta ya Maji. Idara ina watumishi 4 ambao ni waajiriwa ikilinganishwa na mahitaji halisi ya watumishi 21. Upungufu huo wa jumla ya watumishi 17 unapunguza kasi na ufanisi katika utoaji wa huduma ya Maji. Maombi kuonesha hitaji la watumishi wapya yamewasilishwa TAMISEMI na ufuatiliaji unaendelea.