Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Mji Kasulu mkoani Kigoma limempongeza Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Mwl, Vumilia Simbeye kwa kuvuka malengo ya ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa asilimia 102 sawa na zaidi ya Bilioni 2.2 ya makisio na makadilio kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Mji Kasulu Mh, Selemani Kwirusha ametoa pongezi hizo katika mkutano wa baraza la madiwani katika robo ya tatu kipindi cha Januari mpaka Machi kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Halmashauri hiyo mpaka sasa imekusanya zaidi ya shilingi bilioni 2.2 sawa na asilimia 102 ambapo mapato hayo yatasaidia kwa shughuli za maendeleo katika sekta ya elimu, afya na miundombinu ya barabara.
Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Mwl, Vumilia Simbeye amesema mapato hayo yameongezeka kwasababu ya umakini wa ukusanyaji wao wa mapato.Pia amesema mapato hayo yataendelea kuongezeka zaidi kutokana na muda wa ukusanyaji wa mapato bado upo.
Baadhi ya madiwani wanaeleza siri ya wao kuvuka malengo ya ukusanyaji wa mapato hayo kabla hata ya mwaka kutamatika hatua ambayo imekuwa changamoto katika halmashauri nyingine wao wamewezaje.