HALMASHAURI YA MJI YAVUKA LENGO LA UTOAJI WA CHANJO YA POLIO KWA AWAMU YA KWANZA
Zaidi ya watoto Laki tatu na elfu hamsini wenye umri chini ya miaka 8 Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma wanatarajiwa kupatiwa chanjo ya polio awamu ya pili ili kuwakinga na ugonjwa wa polio.
Hayo yalisemwa na kaimu mkuu wa wilaya ya kasulu Bi.Theresia Mtewele ambaye ni katibu tawala wilaya ya kasulu kwenye ufunguzi wa kikao cha maandalizi ya kampeni ya chanjo ya ugonjwa wa polio kwa awamu ya pili yatakayofanyika novemba 02 hadi 05 mwaka huu na kusema,”tujitahidi kuwaelemisha jamii waelewe kuwa hizi chanjo ni salama na zipo kama chanjo nyingine zote za kila siku wanazopata watoto kwahyo wazazi wawaruhusu watoto wapate chanjo kwaajili ya ustawi wa afya zao.
Kwa upande wake mratibu wa chanjo halmashauri ya Kasulu Mji Bi Happyness Itumbe Munisi amesema tayari wamepokea chanjo ya matone ya polio kwa awamu ya pili ambapo kwa awamu ya kwanza waliweka lengo la kuchanja watoto 86,760 ambapo wamechanja watoto 112,053 huku wakiwa mamevuka lengo kwa kupata asilimia 129 katika chanjo ya awamu ya kwanza
Idadi ya watoto wanaokwenda kupatiwa chanjo ya awamu ya pili ni wenye umri chini ya miaka 8 ambao idadi yao ni 112,053 na zoezi hili litafanyika kwa mikoa ya Rukwa, Katavi, Songwe, Mbeya, Kigoma na Kagera.