Mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanali Isaac Mwakisu amewaomba viongozi wa dini zote wilayani humo kuhubiri amani kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 na kuhamasisha waumini kujiandikisha katika daftari la orodha ya mpiga kura linalotarajiwa kuanza Oktoba 11 mpaka 20 mwka huu.
Ameyasema hayo leo aliposhiriki katika kikao cha maridhiano ya amani kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa wiliya kikiwahusisha viongozi wa dini zote toka madhehebu mbali mbali na kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya pamoja na wajumbe wengine.
Mwakisu amesema anatazamia uchaguzi huo kuwa wa amani na utulivu huku akisisitiza watu kupigana kwa hoja zenye nguvu pale inapobidi na kukosoana kiungwana ili kuepuka vurugu zisizo za lazima.
Aidha ameeaeleza viongozi hao kuwaeleza wananchi utofauti wa uchaguzi huu wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu utakaofanyika Mwaka kesho ikiwemo ile ya vitambulisho vya kupigia kura kutotumika katika uchaguzi wa mwaka huu.
Pia amewataka wenye mamlaka ya kutoa elimu ya uchaguzi kutoa taarifa sahihi ili kuepuka taarifa zisizo na ukweli kuenea kwa wananchi na kuleta hali ya taharuki.
Upande wake muwasilishaji wa agenda ya uchaguzi katika kikao hiko amesema kwa upande wa wilaya wamehakikisha ulinzi na usalama unaboreshwa katika kipindi hiki chote cha uchaguzi pia ameeleza umuhimu wa kujiandikisha ikiwa pamoja na kutambulika kwa makazi ya mpiga kura.
Pia ameelezea kuwa kuhakikusha kunakua na Demokrasia na kufuata 4R za Dkt Samia katika zoezi hili tabia zote mbaya za awali zimekomeshwa ikiwemo ile iliyolalamikiwa ya wasamamizi kutokuonekana kwenye vituo wakati wa kurudisha fomu za kugombea
.