Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji-Kasulu amewataka watumishi wa Halmashauri ya Mji kasulu kusimamia miradi ya maendeleo kwa kuzingatia misingi na taratibu zote za utumishi wa umma hasa kwenye masuala ya usimamizi wa Miradi ya Maendeleo.
Hayo yamebainishwa leo tarehe 12, August 2021, kwenye kikao cha makabidhiano kati ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu Bi.Fatina H.Laay na Dollar Rajabu Kusenge aliyeteuliwa na Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji-Kasulu.
Bw.Rajabu kusenga amewataka watumishi wa Halmashauri ya Mji-Kasulu kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni na taratibu za utumishi wa umma hasa kwenye masuala ya makusanyo ya mapato ya ndani na usimamizi wa Miradi ya Maendeleo.
Alieleza kuwa ni suala la usimamizi wa Miradi ya Maendeleo pamoja na kutenga fedha za wanawake vijana na walemavu kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri, litaendelea kupatiwa kiupambe kwani ni jambo la Msingi kwenye maendeleo ya wananchi.
Bi.Fatina H.Laay pia ametumia muda huo kuwashukuru wananchi na watumishi wote alioshikiliana nao katika suala zima la usimamizi wa shughuli za Maendeleo tangu mwaka 2015 hadi 2021, kabla ya kupata uteuzi na kuwa Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Bukoba.
Pia Bi.Fatina Amewataka watumishi wa Halmashauri ya Mji-Kasulu kuonyesha na kumpatia ushirikiano wa kutosha Mkurugenzi Mpya ndg.Dollar Rajabu Kusenge ambaye ameteuliwa ili kuwa Mkurugenzi wa Mji-Kasulu kama walivyompatia ushirikiano kwenye kipindi chake cha miaka 6 aliyotumikia Mji-Kasulu.