Mbunge wa jimbo la Kasulu mjini ambae ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu) Joyce Lazaro Ndalichako amekabidhi gari la kubeba wagonjwa katika kituo cha afya Kiganamo na gari la utawala katika kada ya afya ya Halmashauri ya Mji kasulu na vifaa vingine vya kutolea huduma kituoni hapo pamoja na vifaa wezeshi vya kutembelea kwa baadhi ya watu wenye ulemavu kwa lengo la kutatua changamoto zinazowakabili.
Akizungumza katika hafla fupi ya ugawaji wa vitu hivyo iliyofanyika Februari 19, Ndalichako amesema hayo ni matokeo ya juhudi kubwa zinazoonyeshwa na Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hasani katika kuwafikia wananchi wake na kutatua kero zinazowakabili.
“Daktari Samia anatambua umuhimu wa kuwekeza katika miundombinu na kwa upande wa afya hajatusahau na tayari tumekamilisha zahanati 8 na vituo vya afya 3 pamoja na jengo la wagonjwa mahututi lililogharimu million 250 katika hospitali ya wilaya na katika mwaka huu wa fedha serikali imetenga kiasi cha million 900 kufanya ukarabati mkubwa”
Aidha katika taarifa fupi iliyoandaliwa na kusomwa na katibu wa afya halmashauri ya mji Kasulu Nyangeta Majami imesema; halmashauri imefanikiwa kuanza kutoa huduma katika vituo vya afya viwili na zahanati tano.
Mbali na hayo Mh. Ndalichako amegawa fimbo 20 kwa watu wasiona viti mwendo mashuka ya hospitali pamoja na kutembelea wodi ya wazazi kituoni hapo.