Akiwa katika ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo iliyopo Halmashauri ya Mji Kasulu kuona utekelezaji wa ilani Katibu wa CCM Mkoa Ndg Christopher Palanjo amesema kati ya miradi yote aliyotembelea Wilayani Kasulu hakuna mradi mkubwa na wenye thamani kubwa kama mradi wa maji wa miji 28 uliyopo Halmashauri ya Mji Kasulu.
Aidha ndugu Tamim ameongeza kusema mradi huu mkubwa unaotekelezwa kwa thamani ya Tsh Bi 35 ukikamilika tatizo la maji katika Mji wa Kasulu wote na viunga vyake litakua limekwisha.Hii inaonyesha dhamira ya dhati ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya kumtua mama ndoo kichwani ikitimia kwa wana Kasulu.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini Prof.Joyce Ndalichako amemshukuru Mheshimiwa Rais na kusema mradi huu ukikamilika utafanya upatikanaji wa maji mjini Kasulu kufikia 98% na kuhudumia kata 12 kati ya kata 15.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu Mwl Vumilia J Simbeye ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa niaba ya wananchi wote wa Mji wa Kasulu na kusema mradi huu ni mkombozi wa wananchi waliokua na tatizo kubwa la huduma yam aji kwa muda mrefu.