WADAU WA MAENDELEO MJINI KASULU KUENDELEA KUSAPOTI SEKTA YA ELIMU
Mwenyekiti wa huduma za jamii na diwani wa kata ya mwilamvya mheshimiwa Emanuel gamuye amewashukuru wadau wa maendeleo kwa kuendelea kuchangia sekta ya elimu.
Aliyasema hayo wakati akimkabidhi mwalimu mkuu wa shule ya msingi kalema Bi, Mariam Abdalah Kondo mifuko 30 ya saruji ambayo imetolewa na mdau wa maendeleo kwa ajili ya kusapoti ujenzi wa bweni la watoto wenye mahitaji maalumu ambao wengi wameshindwa kufika shuleni kutokana na umbali
Aidha mkurugenzi wa halmashauri bw.Dollar Rajab Kusenge alisema,”ninaendelea kusimamia uboreshaji wa sekta ya elimu kwa kuboresha miundo mbinu ya ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi na walimu ambapo halmashauri imechangia mawe pamoja na kokoto”.