Wananchi wa Halmashauri ya Mji kasulu mtaa wa Tulieni waaswa kutunza vyanzo vya maji hasa waliopo kando kando ya mto chogo.
Hayo yamesemwa na Afisa mazingira Wambura Niko Halmashauri ya Mji Kasulu baada ya kukutana na baadhi ya wakazi wa mtaa huo waliokua wakiendelea na shughuli zao za ufyatuaji wa matofali katika kingo za mto huo.
Amesisitiza pia kuzingatia shughuli zozote za kibinadamu Kama kilimo zisifanyike katika mazingira hayo ndani ya mita 60.
“Kutunza vyanzo vya maji kunatupa maji safi, tunalinda viumbe hai, na tunapunguza athari za mafuriko.”
Kwa upande wa wakazi wa eneo hilo wameahidi kutekeleza maelekezo yake kwa vitendo na kuunda vikundi vya kijamii vya kutunza vyanzo vya maji, kulinda mazingira kwa ajili ya vizazi vijavyo.
Nae Mtendaji wa kijiji Benedict Batenda Paul aliongeza kuwa mto Chogo ulikuwa na kiwango kidogo cha maji kipindi cha nyuma kutokana na shughuli za kibinadamu kama kilimo na ufugaji kutokana na jitihada za serikali za haraka kutoa elimu kwa wananchi juu ya utunzaji wa mto huo.
“Mpaka sasa ukiona mto Chogo maji yanatiririka baada ya kupanda miti rafiki wa maji na kufyeka miti isiyo rafiki. Hizi zote ni jitihada za serikali katika kutunza maji yetu,” alieleza mtendaji.