Shirika la VERITAS linaloshughulikia haki za wanyama wakishirikiana na Idara ya kilimo, mifugo na uvuvi Halmashauri ya mji kasulu wametoa elimu kwa wananchi wakiwemo wanafunzi na wafugaji wa mbwa na paka juu ya namna nzuri ya kuishi na wanyama hawa ikiwa ni pamoja na kujali afya zao kwa kuwapatia chakula na chanjo.
Akizungumza wakati wa mafunzo yaliyofanyika katika shule ya Nyantare leo hii Selemani Munisi afisa mifugo ameelekeza namna nzuri ya kuhudumia na kutunza mifugo kama mbwa kuwa wanastahili kupata chanjo na dawa kila ili kuwakinga na magonjwa yatokanayo na mifugo hiyo ikiwemo kichaa cha mbwa pia amewaomba kuendelea kuwafadhili katika kutoa elimu.
“Natoa wito kwa VERTAS kuendelea kutoa ufadhili ili kutuwezesha kufikia kata zote za Halmashauri ya Mji wa Kasulu kwani mpaka sasa tumefanikiwa kuzifikia kata tatu tu kati ya kata kumi na tano zilizopo”.
Aidha kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha kilimo mifugo na uvuvi wa Halmashauri ya Mji kasulu Dkt Sudi amewataka wananchi wanaotaka kufuga paka na mbwa kuhakikisha wanafata kanuni za ufugaji ili kuepusha madhara yatokanayo na wanyama hao,lakini pia ameonya tabia ya kuacha wanyama hao kuzagaa hovyo mitaani kitu ambacho kinaweza kuhatarisha maisha ya watu.Aidha ametoa wito kwa VARITAS kuendelea kutoa msaada huu ili elimu hii iweze kufikia maeneo mengi zaidi.
Katika zoezi hilo la utoaji elimu ambalo pia liliambatana na utoaji wa chanjo za mbwa afisa kutoka VERTAS ametoa wito kwa wananchi kuona umuhimu wa elimu wanayoitoa na kwamba elimu hii ni faida kwao wenyewe na hivyo wazingatie elimu hiyo na kuhakikisha wanatekeleza maelekezo waliyopewa hasa namna ya kuishi na wanyama,kuwapenda na kuwapa chanjo.