WANANCHI WAASWA KUPINGA VITA RUSHWA MAADHIMISHO YA MIAKA 61 YA UHURU
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mh Thobias Andengenye amewataka wananchi kupinga vitendo vya rushwa na ubadhilifu ili kuhakikisha wanaendelea kulinda uhuru wan chi yetu
Hayo yamesemwa na mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanal Michael Jastine Ngayalina kwenye madhimisho ya miaka 61 ya uhuru ambayo kimkoa yamefanyika wilayani kasulu na kusema”serikari inaweka fedha nyingi kwa aajili ya miradi ya maendeleo sisi sote ni wafadika wa miradi hiyo tusiseme miradi hii ni ya viongozi tu kila moja awe muwajibikaji katika kusimamia miradi ya maendeleo ,tupinge sana rushwa na vitendo vyovyote vya ubadhilifu ili kuhakikisha miaka 61 ijayo inakuwa ya matumaini na mafanikio kwani vitendo hivyo vinaleta maendeleo ya wasiwasi na miradi kutokukamilika kwa wakati”.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Bw.Albert Msovera amesema “nawashukuru viongozi wa wilaya kwa maandalizi mazuri mliyoyafanya na kuipongeza serikali kwa jitihada mbalimbali inayoendelea nazo za kuboresha maendeleo na inaendelea kufanya kazi kutokana na upatikanaji wa fedha na mipango pia kuwataka watumishi wa Mkoa wa Kigoma kusimama katika nafasi zao ili kutoa huduma stahiki kwa wananchi”.
Aidha Afisa Maendeleo wa halmasahuri ya Mji Kasulu Bw.Nurfus Aziz Ndee amesema”Tangu kuanzishwa kwa halmashauri hii mwaka 2015 mpaka sasa sekta ya elimu,afya kilimo na mazingira vimeborwshwa kwa asilimia 98tangu kuanzishwa kwake hivyo mgeni rasmi ni hatua tumepiga na nasilimia kubwa ya utekelezaji wa miradi yote umetokana na mapato ya ndani”.