Wazazi wa Halmashauri ya mji Kasulu waipongeza serikali ya awamu ya sita kupitia kwa Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kupunguza msongamano wa wanafunzi wa shule ya msingi Kasulu na kuhamia shule mpya ya msingi Murusi.
Wakizungumza shule hapo Leo hii wamesema shule hiyo mpya ya Murusi Imeweza kupunguza mrundikano wa wanafunzi walikua katika shule ya msingi Kasulu na kusema kuwa itasaidia wanafunzi kukaa kwa uhuru darasani na kuzingatia masomo yao.
Janet Ndemeye Amesema kuwa "Kwanza nipende kuchukua nafasi hii kupongeza Rais Dkt. Samia kwa kutujengea hii shule mpya na nafurahi mjukuu wangu kusomea katika shule hii nimekuja kumuaandikisha darasa la kwanza"
Akiongeza Gozbert Erasto amesema" nasikia fahari mwanangu kuhamishiwa katika shule hii Mpya yenye miundombinu mizuri awali mwanangu alikua katika shule ya msingi Kasulu lakiki Sasa hivi darasa la pili kuhamishiwa huku Murusi pia nitoe pongezi za dhati kwa Rais wetu kwa kuwekeza katika miundombinu ya elimu na sisi kama wazazi tunamuahidi kuitunza.
Aidha kwa upande wake Afisa elimu kata ya Murusi Gervas Edward Lugeze Amesema anaipongeza serikali kwa kusimamia ilani ya Chama kwa kuhakikisha miradi iliyopangwa kutekeleza inakamilika.
"Leo nimekuja kukagua hii shule mpya ambayo imejengwa imegharimu kiasi cha Tsh 361,500,000 ikiwa na madarasa ya mfano ya awali pamoja na shule ya lakini pia kukamilisha shule hizi mpya Mfano katika shule hii ya Murusi imeandikisha wanafunzi wapya wa darasa la awali na la kwanza kuanzia darasa la pili wamehamishwa toka shule ya kasulu.”
Ikumbukwe kuwa shule ya msingi ya Murusi imejengwa kwa fedha za Mradi wa BOOST 2022/23 ambapo mpaka imekamiliaka imegharimu kiasi cha milioni mitatu sitini na moja na laki tano ikiwa na vyumba tisa vya madarasa mawili yakiwa ya mfano ya awali, vyoo pamoja na jengo la utawala na tayari madarasa yake yameanza kutumika katika muhula huu wa masomo 2024.