HALMASHAURI KUPINGA UKATILI ALBINO
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa kasulu Dr,Sudi kundelya ametoa wito kwa wananchi kutowanyanyuapaa na kuwaficha walemavu wa aina ili kuweza kuwasaidia katika kupata haki zao za msingi ikiwa ni pamoja na kuwapeleka idara ya ustawi wa jamii kwaajili ya kutambulika,
Ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya sikuya kitaifa ya kuongeza uelewa kuhusu ualbino ambayo yalifanyika katika viwanja vya shule ya msingi nyasha kata ya nyasha na kusisitiza wananchi kuacha kunyanyapaa watu wenye ulemavu hasa albino na kuahidi kama halmashauri kuwasaidia kupata ofisi pia kuwasisitiza wananchi kujitokeza agosti 23kuhesabiwa katika sense ya watu na makazxi ili kuisaidia serikali kupata takwimu sahihi katika kuleta maendeleo.
Aidha Diwani wa kata ya Nyasha bw.Patric Madaraka amewaasa wananchi wa kata hiyo kuendelea kupinga ukatili wa albino hasa kwa kuondokana na Imani potofu za kishirikina ambazo ndio zimekuwa zikichochea ukatili huo na kuwataka kutoas taarifa pindi wanapoona dalili au ukatili ukifanyika
Kwa upande wake Mwnyekiti wa Chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi Albino (TASI) bwana ameimeiomba serikali pamoja na wadau mbalimbali kuendelea kutoa sapoti kwa kuwasaidia walemavu hao katika Nyanja mbalimbali,kama elimu,afya na maradhi.na kuwa licha ya kuendelea kupata misaada kutoka kwa wadau mbalimbali bado wanakabiliwa na changamoto ya ajira kwa watu wenye ualbino hivyo kuiomba serikali kuwasaidia ajira kwa urahisi ili kuwerza kuzitumikia fani walizokuwa nazo.