Katika kikao chake cha kujadili taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi 2020-2025 ya Wilaya ya Kasulu kipindi cha kufikia February, 2025 Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi imeridhishwa na utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Kikao hicho kilichofungulia na Mwenyekiti wa CCM Wilaya Ndugu Mbelwa Chande kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Mji Kasulu na kuhudhuria na wajumbe kutoka Halmashauri ya Mji Kasulu Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali Mkuu wa Wilaya ya Kausu Col. Isaac A. Mwakisu amesema miradi iliyotekelezwa kwa ufanisi katika Wilaya ya Kasulu ni pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika miradi ya kilimo ambapo Wilaya ya Kasulu imeendelea na kunufaika na pembejeo zilizo na ruzuku ya Serikali.
Jumla ya tani 55,081.9 za mbolea zenye ruzuku ya Serikali imetolewa kwa wakulima 95,528 waliosajiliwa kwenye mfumo wa kielettroniki kwa msimu wa kilimo wa 2020-2025 Katika Mwezi Februari 2025.
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF, Wilaya ya Kasulu imetekeleza Mpango wa kunusuru kaya maskini kupitia Tasaf ampapo katika kipindi cha mwaka 2020-2025 hadi kufikia mwezi Februari 2025 kwa kusimamia kasi ya utekelezaji kwa kipindi kipindi cha awamu ya tatu ya TASAF III ili kuwafikia wananchi maskini katika mitaa 108 na vijiji 61 Halmashauri ya Mji kwa kutekeleza miradi ya ajira za muda, kukuza uchumi wa kaya na kuendeleza rasilimali watu.
Miradi mingine iliyotekelezwa ni pamoja miradi ya Nishati ya umeme, maliasili,Ardhi,Miradi ya Elimu, Huduma za Maji na Afya.
Akihitimisha uwasilishaji wake Col.Mwakisu amesema Uongozi wa Wilaya ya Kasulu unatoa shukrani za dhati kwa Serikali Kuu, Taasisi za Serikali, Serikali za Mitaa, Wadau wa Maendeleo, Wananchi, Sekta binafsi, Masirika yasiyo ya Kiserikali kwa mchango na ushirikiano mkubwa walioupata katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi kwa kipindi cha 2020-2025 kufikia Mwezi February 2025.
Akifunga kikao hicho Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya Ndugu Mbelwa Chande amepongeza Wakurugenzi wa Wilaya zote mbili za Kasulu Mji na Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu kwa usimamizi mzuri wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi na kwamba Wilaya ya Kasulu haina deni tena kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.