Halmashauri ya Mji Kasulu kwa Mwaka wa fedha 2024/2025 ilitenga jumla ya Sh: 267,530,060.53 kwa ajili ya ukopeshaji kwa Wanawake, Vijana na Watu wanaoishi na ulemavu.
Akizungumza Mbele ya Mgeni Rasmi leo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu Mwalimu Vumilia Julius Simbeye amsema hadi kufikia Robo ya pili mwaka 2024/25 Halmashauri iliweza kupokea maombi ya vikundi saba (7) ambavyo ni:-
TUJIKOMBOE WANAWAKE – Kata ya Murusi ,NTIHALIZWA WANAWAKE – Kata ya Murusi ,TULASHISE WANAWAKE – Kata ya Murusi,ZASHAKA WANAWAKE – Kata ya Kumnyika,MUMIKI – Kata ya Kigondo, JAKAENUSE – Kata ya Murusi,CHIMPAYE – Kata ya Kumnyika ambavyo vyote jumla vimepokea jumla ya shilingi za Kitanzania milioni thelathini nanne lakisita na kumi na nne elfu.(34,614,000.00)
Simbeye amesema vikundi hvyo vitano vinakwenda kunufaika na mikopo kwa awamu hii baada ya kukidhi vigezo
Naye Mgeni rasmi ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu Mheshimiwa Noel Hanura amewaelekeza wanufaika hao kuitumia mikopo hiyo vizuri na kwa miradi waliyoibuni wao na kwamba nia na madhumuni ya mikopo hiyo ni kuwanufaisha wanakikundi na kusema ikazae maana wamepewa mbegu ili zikazae na wengine wakanufaike na mikopo hiyo baada ya wao kurejesha mikopo hiyo kwa wakati.
Aidha katika shukrani zao wanufaika hao wamemshukuru sana Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan kwa kuviwezesha vikundi hivyo kupata mikopo hiyo.