KATA KUMI NA TANO ZA HALMASHAURI YA MJI WA KASULU KUNUFAIKA NA MIRADI MYA MAENDELEO ITOLEWAYO YA SERIKALI IKIWEMO KATA YA KUMNYIKA
Halmashauri ya Mji wa Kasulu imelishukuru shirika lisilo la Kiserikali la HELPAGE kwa kutoa Ruzuku pamoja na kutenga bima ya afya kwa walengwa walioko kata ya kumnyika
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo BW.Dollar Rajab Kusenge wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya fedha za ruzuku kwa wazee,walemavu na wenye mahitaji maalumu yaliyofanyika katika ofisi ya kata ya kumnyika na kuwataka walengwa hao kutumia Ruzuku hizo kwa malengo yaliyokusudiwa.
Aidha Kusenge amesisitiza kuwa ‘leo tunapewa pesa za ruzuku na kimsingi ni kidogo kwa ajili ya wazeewetu,walemavu lakini na watu wenye uhitaji maalumu hivyo ikawasaidie kutimiza lengo la ruzuku hizo ambayo pia itakuwa na bima ya Afya.’
Zaidi ya kata kumi na tano zilizoko halmashauri Mji wa Kasulu zitanufaika na miradi mbali mbali itolewayo na serikali kama zahanati na shule na hivyo kata ya kumnyika kuwa miongoni mwa wanufaika hao nah ii imetokana na juhudi za ufuatiliaji na utendaji kazi mzuri wa diwani wa kata hiyo bw.Selemani Kwirusha ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kasulu.