BARAZA LA MADIWANI LAKITAKA KITENGO CHA FEDHA NA UHASIBU HALMASHAURI YA MJI KASULU KUTOA ELIMU YA ULIPAJI KODI KWA MFUMO MPYA WA UKUSANYAJI MAPATO(TAUSI)
Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa kasulu mheshimiwa Noel Hanura amewataka kitengo cha fedha kuendelea kutoa elimu ya ulipaji wa kodi kwa mfumo mpya wa tausi kutokana na kukaa muda mrefu bila wafanyabiashara kulipia mapato ya halmashauri.
Aliyasema hayo wakati wa kikao cha robo cha madiwani na kusisitiza,”mnatakiwa kutoa elimu ya mfumo wa TAUSI kwa haraka kwani kwa kipindi cha miezi mitatu halmashauri imepoteza mapato na tukawaeleshe wafanyabiashara ili tutakapoenda kukusanya mapato kusitokee kutokuelewana na kusababisha taharuki kwa wananchi”.
Aidha katika baraza hilo kulifanyika uchaguzi wa makamu mwenyekiti na mheshimiwa Selemani Jonas Kwirusha ambaye ni Diwani wa kata ya Kumunyika kupitia chama Cha Mapinduzi CCM alichaguliwa kwa kupata kura 18 Kati ya 19 na kuwa makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Mji kasulu
Diwani Selemani Kwirusha Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo aliyechaguliwa ametoa neno la shukrani kwa wapiga kura wote waliomchagua na yule ambaye hakumchagua kwa kusema kuwa uchaguzi ulikuwa mzuri na wa demokrasia.
Makamu Mwenyekiti huyo aliyechaguliwa Mwaka huu atahudumu kwenye nafasi yake ya uongozi ndani ya mwaka mmoja Licha ya kuchaguliwa kwa Makamu huyo zimechaguliwa kamati mbalimbali ikiwemo kamati ya maadili ,kamati ya fedha pamoja na kamati ya afya na ukimwi
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kasulu Mji Dollar Rajab Kusenge ametoa matokeo ya uchaguzi huo wa Kumpata Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo katika kikao Cha baraza la madiwani na kusema,” ni kura moja ndiyo iliyoharibika Kati ya kura 19 za wajumbe wa uchaguzi huo na kuwasisitiza kutoa ushirikiano kwa viongozi waliochaguliwa”.