MPANGO WA KUSAJILI NA KUTOA VYETI VYA KUZALIWA WAZINDULIWA HALMASHAURI YA MJI KASULU
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu Mheshimiwa Noel Hanura Buliho ametoa rai kwa Wananchi wa wa Mji Kasulu kujitokeza kwa wingi kuwasajili watoto wenye umri wa chini ya miaka 5 ili waweze kupata vyeti vya kuzaliwa kwani vitawasaidia kwa maisha ya baadae.
Aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa zoezi la usajili vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya miaka 5 na kusema,”naishukuru serikali kwa kuleta mpango huu katika eneo letu kwani utaleta mabadiliko chanya katika maswala ya usajili kwani kwa miaka iliyopita kupata cheti cha kuzaliwa ilichukua takribani miezi sita na sasa tumeona maboresho haya yanavyoleta mapinduzi makubwa “.
“ili mpango huu ufanikiwe ni muhimu tufanye uhamasishaji wa wananchi na kuhakikisha wanapata ujumbe sahihi kwamba uwepo wa mpango huu wa kutoa vyeti ni halali na watoto watavitumia muda wote wa maisha yao na pia nawashukuru wadau wa maendeleo shirika la watoto la uoja wa mataifa UNICEF Serikali ya Canada ,kampuni ya simu za mikononi ya TIGO ambao mmeshirikiana na serikali kupitia RITA kuhakikisha utekelezaji wa mkakati huuunaendelea kutekelezwa tunatamini sana kazi mnayoifanya katika nchi yetu”,aliendelea kusema Hanura.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya mji kasulu bw.Dollar Rajab Kusenge amesema,”tumezindua mpango wa usajili kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano ambao lengo lake ni kumwezesha kila mtoto aliyepo katika eneo letu anasajiliwa na kupata cheti cha kuzaliwa hivyo watakaosajiliwa wawe watu sahihi wenye umri wa chini ya miaka 5 na sitarajii watu wenye umri uliozidi kuja hapa na kutaka kupitia zoezi hili na wao wapate cheti na chimbuko la mpango huu ni kutokana na kwamba idadi kubwa ya wananchi hawajasajiliwa hawana vyeti vya kuzaliwa”.
Nao baadhi ya Wazazi waliofika katika kituo cha afya kiganamo kwa ajili ya kuwasaidia watoto wao waweze kupata vyeti vya kuzaliwa Bi Agnes Honkonya na bw. Revocatus John wamesema,”tunaishukuru serikali ya awamu ya sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha wananchi wa kasulu kuweza kupata vyeti vya kuzaliwa bure bila malipo vitawasaidia watoto wetu kwenye elimu ,afya na mikopo na pia hata kutuondolea ule usumbufu wa kufuatilia vyeti kwa muda mrefu tunawasihi wananchi wenzetu tujitokeze kwa wingi ili tuwaajili watoto wetu wapate vyetivya kuzaliwa”.
Katika zoezi hili halmashauri ya mji wa kasulu tunategemea kuwa sajili watoto 34,437 walio na umri chini ya miaka mitano na hawana vyeti vya kuzaliwa na zoezi hili litakamilika ndani ya siku kumi na nne na kutakuw ana vituo vya usajili 37 ambapo 15 ni ofisi za watendaji kata na 22 ni vituo vya tiba.