HALMASHAURI KUBORESHA HUDUMA YA CHAKULA MASHULENI
Idara ya elimu msingi na sekondari za halmashauri ya mji wa kasulu imetakiwa kuhakikisha zinasimamia upatikanaji wa chakula shuleni.
Hayo yalisemwa na mkurugenzi wa halmashauri ya mji bw.Dollar rajabu kusenge wakati wa kikao cha kamati ya lishe ambacho lengo lake ilikuwa ni kujadili utekelezaji wa shughuli za lishe kwa kipindi cha robo ya tatu januari mpaka machi 2023.
Aidha kusenge ameendelea kuwasisitiza idara ya elimu kuhakikisha shule zilizobaki na hazitoi chakula ndani ya siku 21 ziwe zimeshaanza kutoa chakula na kila idara ihakikishe imechangia nafaka kwa aajili ya kusapoti lishe mashuleni na kumuunga mkono mkurugenzi ambaye naye amechangia nafaka pia.
Kwa upande wake Afisa elimu msingi wa halmashauri bw. Julius buberwa alisema “wazazi wengi wamekuwa wazito katika kuchangia chakula mashuleni hivyo tuendelee kutoa elimu kupitia njia mbalimbali kama mikutano ya hadhara na vyombo vya habari ili waweze kutambua umuhimu wa lishe