Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Isaack Mwakisu, amekutana na viongozi wa dini wa madhehebu ya Kikristo na Kiislamu kujadili maandalizi ya uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 29 Oktoba 2025.
Akiwaongoza kikaoni, Kanali Mwakisu amesisitiza umuhimu wa amani, utulivu na mshikamano wakati wote wa uchaguzi, akiwataka viongozi wa dini kuendelea kuhubiri amani na kuepuka upotoshaji wa mitandaoni.
“Tumejipanga kuhakikisha hakuna atakayesumbuliwa siku ya uchaguzi. Amani ya Kasulu lazima idumu,” — Kanali Mwakisu.
Viongozi wa dini wamemshukuru DC Mwakisu kwa ushirikiano, wakiahidi kuwa mabalozi wa amani na kuelimisha waumini kuhusu umuhimu wa kupiga kura kwa utulivu.
Kanali Mwakisu amehitimisha kikao kwa kuwahimiza wananchi wote wenye sifa kujitokeza kupiga kura, akisisitiza kuwa
“Amani ya Kasulu ni jukumu la kila mmoja wetu.”