Shirika lisilo la Kiserikali la “tan zan eye” lilliloanzishwa mwaka 2017 Mkoani Rukwa linalofanya kazi chini ya Kanisa Katoliki nchini limemkabidhi Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa Ndugu Eliasante M. Mboelo vifaa tiba huduma za macho vyenye thamani ya fedha za kitanzania milioni miambili na themanini (280) vitakavyotumika kutoa huduma za afya ya macho Mkoani Kigoma.
Vifaa hivyo vitasambazwa kwenye vituo kumi na nane(18) vya Halmashauri zote za Mkoa wa Kigoma
Hafla hiyo ya kukabidhi vifaa hivyo imefanyika Hospitali ya rufaa ya Kabanga Halmashauri ya Mji wa Kasulu na kuhudhuriwa na Baba Askofu wa Jimbo la Kigoma Rt. Rev J.R. Mlola , Mkurungenzi wa shirika hilo Dr. Karsten Paust pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu Mwalimu Vumilia Julius Simbeye.
Wengine waliohudhuria ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Halmashauri zote za Mkoa ziliwasilishwa na Waganga wakuu wa Halmashauri za Wilaya.
Samb amba na ugawaji wa vifaa hivyo umefanyika uzinduzi wa ujenzi wa kliniki ya macho ampapo ujenzi huo unategemea kugharimu kiasi cha shilingi milioni mianane sabini za kitanzania. Shirika hilo linafanya kazi zake kwenye mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma.
Katika hotuba yake mgeni rasmi Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa Ndugu Eliasante M. Mboelo ameshukuru ushirikiano mkubwa uliopo kati ya Kanisa Katoliki na Serikali na kwamba huduma hizi zinagusa maisha ya watu hivyo kulishukuru shirika hilo kwa msaada huo mkubwa wa vifaa vya kutolea huduma za macho.
Mboelo amesema kuwa hii inaonyesha waziwazi uungaji mkono juhudi za Mh. Rais Samia na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Kazi na Utu,Tunasonga Mbele.”