MWENYEKITI UVCCM AIPONGEZA HALMASHAURI YA MJI KASULU KUSIMAMIA MIRADI YA VIJANA KWA UTOAJI WA MIKOPO YA ASILIMIA 4
Mwenyekiti wa Vijana CCM Taifa Mohammed Ali Mohammed (kawaida) Ameipongeza Halmashauri ya Mji Kasulu kwa kuweza kusimamia miradi ya vijana iliyoanzishwa kwa fedha za mkopo wa asilimia 4 za Halmashauri kwa vijana
Ametoa pongezi hizo wakati akikagua mradi wa kikundi cha Vijana Iposa kalema wakati wa ziara yake wilayani kasulu iliofanyika januari 25 mwaka huu katika eneo la kiwanda cha vijana Iposa pamoja na kuwapongeza Vijana waliofaidika na fedha za mkopo huo huku akieleza zamira za mikop hiyo ni Kuwezsha Vijana kujiajiri na kujipatia kipato wenyewe.
Aidha Ameelezea lengo la Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dokta Samia Suluhu Hassan kusitisha mikopo hiyo ni kufuatilia utekelezaji utaratibu mzuri kuhakikisha Vijana wanaostahili kupata mikopo hio wanaipata
"kwa bahati mbaya Kuna baadhi ya maeneo fedha zilikua zikitumika vibaya Dk Samia akasema anasitisha mikopo ili kutekeleza utaratibu mzuri ili kuhakikisha Vijana wa kimaskini waweze kunufaika na dhamira hiyo bado anayo na anaendelea nayo"
Awali akimkaribisha Mwenyekiti huyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu Dollar Rajab Kusenge Ameelezea namna ya uanzishwaji wa Mradi wa Vijana wa Iposa Kalema ambao wamefaidika kwa kupewa kiasi cha shilingi TShs 125 pamoja na eneo la kuanzisha Mradi huo
"kiwanda hiki wamejenga wenyewe kila kitu kuanzia msingi walianza kupewa elimu kupitia program ya Iposa nami niliwafanyia majaribio ya vitendo mpka walipoweza kufanya kazi tu kawapa pesa"
Kabla ya kusitishwa kwa mkopo wa vijana na Mh Dokta Samia Suluhu Hassan 4% ya mikopo ya halmashauri ilikua inatolewa kwa Vijana kwa lengo la kuwawezesha Kujikwamua kiuchumi na kupunguza changamoto ya upatikanaji wa ajira mchini.