Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefanya ziara ya ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa Halmashauri ya Mji-Kasulu.Katika ziara hiyo amezindua jengo la utawala lililojengwa kwa thamani ya Tshs. Bilioni 3 na Milioni 750 ikiwa ni fedha toka serikali kuu.
Pia amewataka watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu kulitunza ili liweze kudumu kwa kipindi kirefu na amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bi. Fatina H kwa kusimamia mzuri wa matumizi ya fedha za miradi ya Maendeleo.
Hata hivyo amezitaka Wizara zinazohusika na utekelezaji wa Miradi Mbalimbali inayotekelezwa Halmashauri ya Mji kufanya kazi kwa haraka ili kuweza kuondoa kero zinazo wakabili wananchi waishio Mji-Kasulu ambazo ni Ukosefu wa Maji Safi na Salama, Umeme, Afya pamoja na Barabara.
Lakini pia Naibu Waziri wa Nishati Wakili. Stephen Byabato amemtaka Meneja wa Tanesco Wilaya ya Kasulu kuondolewa haraka na kupelekwa mahali pengine ili kuweza kupisha Miradi mbalimbali iweze kuendelea.