Mkuu wa wilaya ya kasulu Kanal Isack Mwakisu aliwataka Madiwani wa halmashauri ya mji kasulu mkoani kigoma kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kutunza mazao ya chakula baada ya mavuno kwa lengo la kuhakikisha jamii haipati shida ya chakula kabla ya msimu ujao wa kilimo.
Aliyasema hayo kwenye kikao cha baraza la madiwani kilichoketi leo tarehe 5 mei 2023 katika ukumbi wa mikutano na kusema,”ni aibu kuona wananchi wanalia njaa hata msimu ujao wa kilimo haujaanza”,baadhi ya wananchi hawatambui umuhimu wa kuweka akiba ya chakula kwa ajili ya familia zao na kukimbilia kuuza mazao yao ili wapate fedha za muda mfupi jambo ambalo linatakiwa kusimamiwa na viongozi wa maeneo yao.
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashuri ya mji mheshimiwa Hanura Buriho alisema ,”sisi kama baraza la madiwani tuko tayari kuwaelimisha wananchi wetu namna bora ya utunzaji wa mazao ya chakula ili iwasaidie wakulima kunufaika hapo baadae.”
Aidha mheshimiwa Hanura aliwasisitiza TANESCO,RUWASA na TARURA kuhakikisha wanaboresha miundo mbinu wananayoisimamia kuwaifikia wananchi kwa urahisi ili kuondoa kero za maji,umeme na barabara hasa kwa wananchi wa kata za pembezoni katika kutekeleza majukumu yao ya kibinadamu.