MAFUNZO USHITIRI KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA
Jumla ya waganga wafawidhi ,watunza stoo na wafamasia 45 wa zahanati, hospitali na vituo vya afya wamepatiwa mafunzo ya siku mbili tarehe 13-14 ya mfumo mpya wa mshitiri.
Hayo yalisemwa na mmoja wa wakufunzi waliokuwa wakitoa mafunzo hayo ambaye ni mratibu wa huduma za maabara bw. Osward Kirula na kusema,”lengo la kuwatoa vituoni na kuwaleta hapa kupata mafunzo haya ni kuwajengea uwezo juu ya mfumo mpya wa kielekroniki wa mshitiri na namna ya kuutumia”.
Aidha kwa upande wao washiriki walioshiriki mafunzo hayo walisema kuwa ,”huu mfumo mpya wa mshitiri utaturahisishia katika upatikanaji kwa urahisi wa maombi ya dawa kwani zamamni tulitumia vitabu ambayo vilichukua muda mrefu hivyo kwa sasa tutatumia muda mchache katika uagizaji na tutatoa huduma kwa urahisi”.