Hayo yameelezwa na washiriki wakati wa mafunzo yaliyofanyika katika Shule ya Sekondari Bogwe kwa kupitia mradi wa Shule Salama yakiwahusisha walimu wakuu na waratibu elimu wa Halmashauri ya Mji Kasulu.
Mafunzo hayo yaliyochukua siku tatu kuanzia tarehe 29/01/2025 yamelenga kuwasaidia viongozi hao kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili katika usimamizi wa ufundishaji na ujifunzaji ikiwa ni Pamoja na kupeana mbinu bora za utatuzi wa migogoro kupitia jumuya zitakazoundwa katika kila kata na kuwapa nafasi ya kukutana na kupeana uzoefu mbalimbali katika kila robo ya mwaka.
Mmoja wa wawezeshaji wa mafunzo hayo Mwl Isaack Manga kutoka Halmashauri ya manispaa Kigoma amesema
Kutokana na uwepo wa changamoto mbalimbali katika shule nyingi Serikali imeona kuna umuhimu wa wakuu wa shule pamoja na waratibu elimu ambao ndiyo wasimamizi hasa wa shughuli zote za ufundishaji na ujifunzaji katika shule kupatiwa mafunzo ya namna ya utatuzi wa changamoto hizo ili kuleta ufanisi.
Kwa upande wake Afisa elimu ya watu wazima Halmashauri ya Mji Kasulu Felician Venance ambaye pia ndiye mratibu wa mafunzo hayo amewashukuru wakufunzi na washiriki wote kwa kuwezesha mafunzo haya na kuwataka kwenda kutekeleza yale yote waliyojifunza ili kuleta mabadiliko chanya.
Aidha akiwakilisha washiriki wote Mwalimu mkuu wa shule ya msingi ameishukuru halmashauri ya mji kwa uratibu mzuri wa mafunzo hayo na kuongeza kua mafunzo ya ujenzi wa mfumo wa uongozi yatawawezesha viongozi hawa kutimiza jukumu lao kuu la kusimamia ufundishaji na ujifunzaji,rasilimali watu,rasilimali fedha na utatuzi wa migogoro mbalimbali ili kuleta mabadiliko Chanya katika eliimu.