MAKARANI WANAOENDELEA KUPATA MAFUNZO YA SENSA WAASWA KUFANYA KAZI YA SENSA KWA UZALENDO NA WELEDI NA UFANISI WA JUU
Makarani wanaopata mafunzo ya sensa wamepewa wito wa kuhakikisha wanatambua wajibu mkubwa walionao katika zoezi la sensa kwa kusikiliza mafunzo kwa umakini na ufasaha kwa maslahi mapana ya Kasulu na taifa kwa ujumla
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya yakasulu wakati alipotembelea kwenye ukumbi wa bogwe sekondari na kusema “ serikali ya awamu wa sita chini ya Mh Raisi Samia Suluhu Hassan inatoa pesa nyingi kwa ajili ya kuhakikisha zoezi hili linakamilika kwani sensa itamsaidia kupanga mipango ya kimaendeleo kwa nchi kwa miaka kumi na kuwasisitiza kufanya kazi hii kwa uzalendo mkubwa ili tufikie hatma ambayo Mh.Raisi anaitaka.”
Kwa upande wake mratibu wa sensa wa halmashauri ya Mji Kasulu Bw. Casmiry Charles amesema, “Lengo kuu la mafunzo haya ni kutoa miongozo na vifaa muhimu ambavyo vitatumika katika zoezi la sensa ya watu na makazi tarehe 23 mwezi wa 8 ili kupata taarifa muhimu za kidemografia,kiuchumi na kijamii katika eneo husika” Mafunzo hayo yamezinduliwa rasmi tarehe 31 julai na kutoa muongozo maalumu wa mafunzo ya sensa kulingana na National Bureau of Statistics NBS ambao unajumuisha mitihani maalumu itakayofanyika tarehe 5 ,tarehe 8 pamoja na tarehe 14 mwezi wa 8 na watakaofaulu katika mitihani hiyo watendelea na zoezi la sensa
Aidha Mkufunzi Ngazi ya Mkoa wa Kigoma na msimamizi ngazi ya Wilaya Kasulu kutoka ofisi ya Taifa ya takwimu Dodoma Bi.Donatha Tenesi amewasisitiza makarani na wasimamizi kuhakikisha ubora wa takwimu na kufuata miongozo kutoka makao makuu ili kusaidia nchi kupata taarifa za takwimu sahihi kwa ajili ya kupanga bajeti na maendeleo ya nchi zitakazotumika kwa miaka kumi.
Kwaupande wa washiriki wa mafunzo hayo wamesema kuwa kuwepo kwa mafunzo haya kutawasaidia kkuweza kufanya kazi kwa weledi na kuahidi kuhakikisha zoezi hili la sensa ya watu wa makazi linafanyika vizuri na kumalizika kwa usalama Zaidi.
Mafunzo haya yatakuwa ya siku 19 yatakayotolewa katika kata 15 za Kasulu ambazo ni kata ya msambara,muhunga,kumnyika,kibondo,murufyiti,murusi,murubona,nyumbigwa,kumsenga,ruhita,kimobwa,heru juu ,nyansha ,muhunga pamoja na mganza