MKURUGENZI ATOA WITO
Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu Bw,Sudi Kundelya amewashukuru shirika la chakula duniani (WFP)kwa kuwa halmashauri imekuwa wanufaika wakubwa kupitia miradi ya KGP inayotolewa na kuendeleza wafugaji wadogo wadogo na wakulima japo mradi unafikia mwishoni tunawashukuru kwa ushirikiano
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake na wawakilishi kutoka WFP ambao walikuwa na ziara ya ufuatiliaji wa miradi inayotekelezwa kupia ufadhili wao tangu 2018 mpaka sasa ambao umewasaidia na kuwajengea uwezo wakulima na wafugaji kuinua kipato na uhifadhi wa mazao na kuongeza kipato kwa halmashauri kupitia ushuru unaotokana na mazao ya mashambani na mapato hayo yamekuwa yakiongezeka mwaka hadi mwaka.
Aidha kwa upande wao baadhi ya wakulima wamesema kuwa mafunzo waliyoyapata kupitia WFP na wanachama wa faida mali ambayo yamewasaidia kuvuna kisasa bila kuchafua mazao hayo na kupata mazao mengi,pia kuwarahisiushia upatikanaji wa masoko kiurahisi na kuinua kipato cha mmoja mmoja licha ya kuwa na changamoto za upatikanaji wamifuko ya kuhifadhia.