Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu bw.Dollar Rajabu Kusenge amefanya ziara ya kutembelea miradi ya Ujenzi wa Madarasa inayoendelea kutekelezwa ndani ya Mji-Kasulu ili kuweza kutoa ushauri elekezi katika utekelezaji wa miradi ya Maendeleo.
Halmashauri ya Mji wa Kasulu inatekeleza ujenzi wa Madarasa 57 kupitia fedha za kupambana na ugonjwa wa COVID 19 iliyotelewa kwaajili ya kupunguza mrundikano wa wanafunzi shuleni.
Alisema ujenzi wa madarasa katika shule za sekondari zilizopo Halmashauri ya Mji-Kasulu unatakiwa kuwa umekamilika ifikapo 10 Desemba 2021 ili kuweza kuweka maandalizi mazuri ya mapokezi ya wanafunzi wanaotegemewe kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2022.
Katika ukaguzi huo kumebainika changamoto nyingi ikiwemo baadhi ya miradi kutekelezwa kwa kasi ndogo jambo ambalo mkurugenzi amewataka mafundi wajenzi Pamoja na walimu wakuu wa shule za sekondari kuongeza kasi katika kusimamia miradi hiyo ya ujenzi wa madarasa ili ifikapo tarehe husika iweze kukabidhiwa.
Bw.Dollar Rajabu kusenge, amewataka walimu kuongeza kasi ya usimamizi wa miradi hiyo ya ujenzi wa madarasa kwa kuzingatia viwango na ubora wa fedha zilizotolewa na serikali kiasi cha shilingi milioni ishrini kwa darasa.
Amesema kwa mkuu wa shule ambaye atashindwa kusimamia miradi ya ujenzi wa mdarasa atamuondosha katika nafasi hiyo ili aweze kupitisha ujenzi wa madarasa uweze kukamilika kwa wakati.