MKAA MBADALA CHACHU MAENDELEO
Wananchi Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma wametakiwa kuongeza kasi ya kuendelea kutunza na kuhifadhi mazingira yanayowazunguka kwa kuepuka kulima karibu na vyanzo vya maji , uchomaji misitu ikiwemo ukataji wa miti ovyo hali inayopelekea kuzorotesha usitawi wa mazingira.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanal Isaac Mwakisu kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira yaliyofanyika leo juni tano mwaka huu kwenye viwanja vya hospitali ya wilaya ya kasulu na kusema takwimu za matumizi ya nishati mbadala yanaongezeka kwa kiwango kidogo sana wilayani humo
Aidha kanal Mwakisu ametoa wito kwa serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo kuelekeza nguvu zao za pamoja kuwasaidia wananchi wenye kipato kidogo ili waweze kumudu matumizi ya nishati mbadala ikiwemo matumizi ya majiko banifu
.
Kwa upande wao wananchi wameishukuru serikali kwa kuendelea kutoa elimu ya utunzaji na uhifadhi wa mazingira na kuwaomba wadau mbalimbali wa maendeleo kuendelea kujitokeza kuhamasisha na kutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa kutunza mazingira kwa manufaa ya vizazi vya sasa na baadae .