MRADI WA SHULE BORA UNALENGA ELIMU KWA WATU WOTE
Mshauri wa elimu kutoka taasisi ya british high commission iliyopo jijini dareslaaam ndugu colin bangay amehitimisha ziara yake mkoani kigoma kwa kukagua namna mrdi wa shule bora unavyotekelezwa.
Akifanya ziara katika halmashauri ya mji aliwataka viongozi wa elimu kuendelea kutatua changamoto mbalimbali zilizopo katika sekta ya elimu kwa kushirikiana na jamii kwa kuendelea kuinua kiwango cha elimu jumuishi kwa kuwatambua watoto wenye ulemavu na kuweka mazingira salama ya kujifunzia kwa wanafunzi wote wakike na wakiume.
Kwa upande wake afisa elimu taluma mkoa wa kigoma ndugu davidi mwamalasi alisema serikali inaendelea kusimamia na kuhakikisha makundi yote yanapata elimu kwa usawa pasipo upendeleo na inaendelea kushirikiana na jamii kuinua viwango vya elimu ,uwepo wa usalama na usawa katika kuhakikisha watoto wote wanapata elimu bora
Aidha mwalimu mtaaluma wa shule ya kabanga mazoezi bi anna dismas alisema katika katika shule hiyo wananfunzi wenye mahitaji maalumu na walimu wa shule hiyo kupitia mradi wa shule bora wamepata mafunzo ya walimu kazini (MEWAKA) ambayo yamewasaidia katika uboreshaji wa ufundishaji na ujifunzaji katika shure hiyo.
Mradi wa shule bora ni mpango wa elimu wa serikali ya Tanzania kwa ufadhili wa UK Aid unaolenga kuunga mkono uboreshaji wa elimu ya msingi Tanzania ukiweka mikakati sahihi na kuhakikisha watoto wote wenye ulemavu ,wanaoishi katika mazingira maguu wasichana na wavulana wanapata wanapata elimu bora.