Naibu waziri wa Tamisemi Mh.David Silinde amethibitisha uwepo wa vyumba vya madarasa 57 vilivyokamilika pamoja na madawati ambavyo vinatumika kwa wanafunzi halmashauri ya mji wa kasulu na kupongeza halmashauri kwa kuweza kusimamia na kukamilisha madarasa hayo kwa wakati.
Ameyasema hayo januari 21 katika ziara ya ukaguzi aliyoifanya katika shule 17 halmashauri ya mji kasulu ambazo zilipata fedha kiasi cha shilingi bilioni 1,140,000,00 zilizotoka mfuko wa fedha wa kimataifa (IMF) ikiwa ni fedha kwaajili ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa uviko 19 na kusisitiza halmashauri kuhakikisha lile lengo ambalo mheshimiwa Rais SAMIA SULUHU HASSAN alilokusudia kuboresha na kujenga madarasa ya kisasa linatimia ikiwa ni pamoja na kuhimiza watoto wote waliochaguliwa kufika shuleni kupata elimu licha ya kukosa sare za shule kwa kuwa serikali iliruhusu mtoto kusoma bila ya kuwa na sare mpaka pale zitakapopatikana.
Aidha Silinde amemtaka mkuu wa wilaya ya kasulu Kanal Isaac Mwakisu kuhakikisha anapata takwimu sahihi ya kwanini idadi ya wanafunzi waliopo niwachache ukilinganisha na serikali iliyowachagua kujiunga na kidato cha kwanza kwa kuwahimiza wazazi kuwapeleka shule watoto wote waliochaguliwa.
Baadhi ya wanafunzi waliojiunga na kidato cha kwanza na wanatumia madarasa hayo wameishukuru serikali kupitia Mheshimiwa RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA SAMIA SULUHU HASANI kwani uwepo wa madarasa hayo umesaidia kuongeza idadi ya shule mpya ambazo zitawasaidia watoto waliokuwa wakitumia umbali mrefu kufuata shule kuweza kupata ufaulu mzuri,kuwaepushia watoto wa kike kukumbana na ukatili wa kijinsia wa aina yoyote waliokuwa wakikutana nao wakati wakienda shuleni ambako walitumia umbali mrefu.
Kwaupande wake mkazi wa kijiji cha marumba kata ya Muhunga bw. Petro kalihadya amesema kuwa ujenzi wa shule hiyo mpya utakuwa umesaidia kwa wanafunzi kupunguza kutumia umbali wa km 25 kufuata shule katani muhunga ambapo ndipo kuna sekondari tegemezi inayohudumia kata nzima yenye wakazi wengi na kugusia swala la serikali kuweka madarasa yenye viti na meza kutasaidia kuboresha elimu kwa watoto wao kutokana na familia nyingi hazikuwa na uwezo wa kupata vifaa hivyo na kuwataka watoto watakaoenda katika shule hiyo mpya inayotarajia kuanza muda wowote kusoma kwa bidii ili kuweza kufika juu Zaidi kielimu.
Hata hivyo mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa kasulu bw.Dollar Rajabu Kusenge amemshukuru Rais SAMIA SULUHU HASSANI kwa kuweza kutoa pesa za ujenzi wa madarasa na shule mpya utaleta manufaa hasa kwa kuwapunguzia adha ya kutembea watoto walioko katika kata za pembezoni mwa mji na kuahidi kuendelea kuhamasisha kaya kwa kaya nakila kata wazazi waweze kupeleka watoto wao shuleni kama maagizo ya naibu waziri wa tamisemi yalivyosema kutokanana kuonekana kwa changamoto ya watoto wengi kutokufika shuleni.
Mkuu wa wilaya ya kasulu Kanal Isaac Mwakisu amesema amepokea maagizo kutoka kwa naibu waziri wa tamisemi na kuahidi kuyafanyia kazi kwa uharaka zaidi na kutoa rai kwa wananchi wote kuhakikisha wanawapeleka watoto wote kujiunga nakidato cha kwanza katika shule walizopangiwa na endapo watakaidi agizo hilo la serikali hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mzazi asiye tekeleza maagizo ya serikali.