Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Col.Isack Mwakisu ameishukuru serikali ya UTURUKI kwa kushirikiana na taasisi ya Rehama WAKFU kwa utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ndani ya Mji wa Kasulu.
Hayo yamebainika wakati wa ziara ya barozi wa Uturuki Novemba 29, 2021 iliyofanyika katika Shule ya sekondari kidyama iliyoko Halmashauri ya Mji wa Kasulu Mtaa wa Kidyama,kata ya Kigondo, imepata msaada wa kisima kirefu cha maji kupitia ufadhi wa serikali ya uturuki.
Taasisi ya Rehama wakfu imetekeleza zoezi la uchimbaji wa kisima kirefu katika shule ya sekondari kidyama, mradi huo unawasaidia wananchi wa kidyama Pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi kidyama ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa wakiteseka na suala la upatikanaji maji.
Wakati wa ziara hiyo,barozi aliweza kuweka jiwe la msingi katika mradi huo wa maji uliopo katika shule ya sekondari Kidyama na Barozi aliwajulisha wananchi Pamoja na viongozi wa serikali kuwa serikali ya uturuki itaendelea kushirikiana na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika utekelezaji wa miradi ya Maendeleo.
Pia mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa kasulu bw.Dollar Rajabu kusenge alitoa pongeza kwa taasisi na serikali ya uturuki kwa kuendelea kufadhili miradi ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya Mji-Kasulu kama mradi huu wa kisima kirefu uliotekelezwa kwa kiasi cha milioni kumi na tano.