Kasulu, 25 Oktoba 2025
Maadhimisho ya usafi wa kila mwisho wa mwezi yamefanyika leo katika Soko Kuu la Kumsenga, yakihusisha viongozi wa Wilaya ya Kasulu, watumishi wa serikali na wananchi kutoka halmashauri zote mbili.
Mgeni rasmi, Ndugu Ibrahim Samson Mwangarume, Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Kasulu, amewataka wananchi na wafanyabiashara kudumisha utamaduni wa kufanya usafi kila siku ili kuepuka magonjwa ya milipuko.
“Ni jukumu letu sote kuhakikisha tunafanya usafi mara kwa mara. Mji safi ni afya na fahari yetu sote,” alisema Mwangarume.
Viongozi wa idara ya usafi na watendaji wa kata wametoa wito kwa wananchi kuendelea kushiriki katika shughuli za usafi na kuhifadhi taka kwenye vyombo maalum, ili kuweka mazingira ya Kasulu yakiwa safi na salama.