UJENZI WA ZAHANATI KILA KATA KUTATUA HUDUMA ZA AFYA KWA WANANCHI
Halmashauri ya mji wa kasulu mkoani kigoma imekamilisha ujenzi wa zahanati mbili katiaka kata ya kumnyika na msambara zenye thamamni ya shilingi milioni 100 na kuweka vifaa tiba kupitia mapato ya ndani ya halmashauri.
Hayo yamesemwa na mkurugezi wa halmashauri ya mji bw.dollar rajabu kusenge kwenye mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi katika kata ya murubona na kusema”kukamilika kwa zahanati hizo kumesogeza huduma za matibabu karibu na kuwa ujenzi huo umeambatana na kuweka vifaa tiba pamoja na samani ili punde zitakapofunguliwa zianze kuwahudumia wananchi ambao wamekuwa wakihangaika kupata huduma hiyo”
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa kata hizo wamesema”kuoneshwa ushirikiano katika miradi ya maendeleo kati ya serikali na wananchi kunarahisisha miradi kukamilika kwa wakati ikiwemo ujenzi wa zahanati hizo”