Uongozi wa chuo cha maendeleo ya wananchi Kasulu wapongezwa kwa usimamizi mzuri wa chuo hicho kinachoonekana kukua kwa kasi na mazingira yake kuendelea kuboreshwa ikiwa ni pamoja na namna wanavyosimamia utoaji wa taaluma chuoni hapo.
Hayo yamesemwa na Mwenyeketi wa bodi ya chuo hicho ambaye ni mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu Dollar Rajab Kusenge wakati akifanya kikao cha bodi kujadili mwenendo mzima wa hali ya maendeleo ya chuo.
Katika kikao hicho kilichofanyika leo hii katika ofisi za mkuu wa chuo amesema anaimani kubwa na uongozi wa chuo kwa namna wanavyosimamia shughuli za uboreshaji wa chuo hicho.
“hatuna wasiwasi na uongozi wa FDC kasulu,chuo kinakua kwa kasi nzuri sana mazingira yanaboreka na uendeshaji uko vizuri ”
Aidha amewashauri kufanya mabadiliko ya kiteknolojia na kutumia zana za kisasa katika kufundisha ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya dunia.
Ameongeza kuwa kwakua dunia inawekeza katika kuvumbua mitambo mbalimbali hivyo wanatakiwa kuandaa vijana ili kuwa na unaoendena na kasi iliyopo ikiwa ni pamoja na kuanzisha kozi fupi za sayansi ya kompyuta na utafiti kwalengo la kufundisha program tofauti zitakazowawezesha kuongeza mapato chuoni hapo.