WADAU WA MAENDELEO KUWASAIDIA WENYE MAHITAJI MALUMU
Wadau wa maendeleo mjini kasulu wameombwa kuendelea kushirikiana na halmashari ya mji katika kuwasaidia watoto ewenye mahitaji maalumu ikiwa ni pamoja na vifaa vya ufundishaji na kujifunzio.
Hayo yalisemwa na mkurugenzi wa halmashauri ya mji bwana dollar rajab kusenge alipotembelea kituo cha watoto wenye mahitaji maalumu ikiwa ni ziara ya kutembelea miradi ya halashauri katika kituo cha kabanga mazoezi kilichopo nkata ya msambara na kusema”watoto hawa wanahitaji kuboreshewa mabweni ,kununuliwa vifaa kama madaftari ,kalamu,mbao za kujifunzia kwajili ya wasio ona,mafuta kwaajili ya watoto wenye ulemavu wa ngozi(albino)hivyo kuwataka wadau kujitokeza kwaajili ya kushirikiana na halmashauri katika kutekeleza jambo hili.
Aidha kwa upande wake mwalimu anayewasimamia watoto hao alisema bado kuna uhitaji wa vifaawezeshi kwa ajili ya ufundishaji na ujifunzaji pia uhaba wa walimu wenye taaluma ya kuwafundisha watoto wenye mahitaji maalumu na kuiomba serikali kuwaboreshea mazingira na kuongeza ajira kwa walimu hii itaongeza ufaulu.