Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu) na mbunge wa Kasulu mjini Mh Joyce Ndalichako Amewataka walimu wa shule za msingi na sekondari wilayani Kasulu kutoa elimu yenye tija kwa wanafunzi. Hayo yamejiri katika kikao cha wadau wa elimu wilayani Kasulu kilichofanyika Januari 20 mwaka huu katika ukumbi wa Chuo cha ualimu Kasulu.
Akihutubia katika kongamano hilo waziri Ndalichako Amesema ni jukumu la walimu kuhakikisha wanasimamia elimu ili kuleta matokeo chanya kwa taifa la Tanzania.
"wanafunzi watoke wakiwa wameiva kwa kweli bila kufanya hivyo tutakua wahujumu uchumi maana tumeletewa hela nyingi tusiposimamia zitakua zimepotea wakati lengo lilikua ni kutengeneza msingi mizuri kwasababu serikali ya Dk Samia Suluhu Hassan inatambua kwamba elimu ndio msingi wa maendeleo yote. "
Aidha Amewataka wakuu wa shule kuwa wabunifu katika mbinu za kutoa chakula mashuleni wakishirikisha wazazi ili kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa. kwa lengo la kutatua changamoto za upatikanaji wa chakula mashuleni. Ameyasema haya baada ya wakuu hao washule kuelezea namna wanavyopata changamoto katika kutoa chakula mashuleni ikiwemo watoto kutokurudi mchana wanapokwenda majumbani kwaajili ya chakula.
Akihitimisha kwenye kongamano hilo mkuu wa wilaya ya kasulu Kanali Isack Mwakisu amewasisitiza walimu kupiga vita vitendo vinavyofaanya na waganga wa jadi maarufu kama kamchape akidai vitendo hivyo hufitinisha serikali na wananchi wake na kwamba serikali haiwajatuma waganga hao kama wanavodai huku ikiendelea kuwachukulia hatua.