Wananchi wa kata ya ruhita iliko halmashauri ya mji wa kasulu wameonywa nan a kuaswa kutokuvamia maeneo ya serikali kwa kufanya shughuli zakibinadamu kama kilimo na ufugaji.
Hayo yalisemwa na mkurugenzi wa halmashauri ya mji kasulu ya mji kasulu bw.Dollar Rajab Kusenge kwenye mkutano wa hadhara wakati akitatua mgogoro wa ardhi uliokuwepo baina ya serikali na wananchi wa kata hiyo.
Aidha Kusenge alisisitiza wananchi kutii sheria bila shuruti kwa kuyalinda maeneo ya serikali kwani katika kata ya ruhita bado kuna uhitaji wa miundo mbinu ya elimu hivyo kuyalinda ni kuweka hazina kwa vizazi vilivyopo na vijavyo na iwapo atatokea mtu sherika kali zitachukuliwa dhidi yake.
Aidha kwa upande wao baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo walisema wameamua kulikabidhi eneno hilo lililokuwa linamilikiwa na kata kwa halmashauri ili liwedhe kulindwa kwani badhi ya wananchi wamekuwa wakivamia kwa kufanya shighuli hizo za kilimo na ufugaji na kujimilikisha pia kinyume cha sheria hali iliyopelekea migogoro mingi kutokea hivyo likiwa chini ya serikali litatunzwa vizuri na kulindwa.