WATAALAM HALMASHAURI YA MJI WAASWA KUTOFANYA KAZI KWA MAZOEA KWANI ITAWAPUNGUZIA WELEDI
Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanal Isaac Mwakisu amewataka wataalamu na watumishikuacha kufanya kazinkwa mazoea kwani kufanya hivyo kunawapunguzia nidhamu na WELEDI kazini.
Aliyasema hayo wakati wa kikao cha ofisi ya Mkuu WA Wilaya na wataalamu hao ambacho lengo lake ilikuwa kukumbushana namna ya kufanya kazi Kufata misingi na maadili ya kiutumishi na kusema,“Ninyi watumishi wa serikali hakikisheni manatunza siri za serikali nanmuwe watiifu ili kufanya kazi Kwa weledi na maadili baadhi yenu hamfanyi hivyo mnatoa Siri za serikali Tu hovyohivyo badilikeni kwani mkifanya kazi hii itapunguza mizigo kwangu ya kitatua Kero ambazo zilitakiwa zitatuliwe ngazi ya chini Kwa watendaji wa kata”.
Aidha Mwakisu ameendelea kuwasisitiza kuwa uwajibikaji Kwa baadhi ya wataalamu hauridhishi kwani wengi wao wanafanya kazi kwa mazoea na kuahidi kuwachukulia hatua nankuwawajibisha wale wote ambao hawatendi kazi Kwa weledi
Kwaupande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Kasulu Bi.Telesia Mtewele alisema,“Kwanza kabisa naomba niwatie Moyo kwani mnafanya kazi vizuri saana na tuendelee kuchapa kazi lakini ofisi yetu haitavumilia Kwa yeyote atakayekiuka misingi ya maadili ya utumishi wa umma naendelea kuwasisitiza watumishi kuacha tabia ya kutoa Siri za serikali kwani nikosa kisheria na pia halmashauri yenu ya mji wa Kasulu unafanya vizuri sana kazi niwaombe tushirikiane”.
Naye Mkurugenzi wa Kasulu Mji Bw.Dollar Rajab Kusenge amesema ,“kwanza nikushukuru Mkuu wa Wilaya na Katibu Tawala Kwa kuweza kufanya kikao na watumishi wangu nimepokea na nakuahidi kuyafanyia kazi maelekezo yote uliyonipatia na majibu nitayawakilisha lakini pia niendelee kuwasisitiza watumishi wenzangu tuendelee kufanya kazinkwa kufuata maadili ya utumishi kwani serikali ya awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu Hassan imetupendelea Kwa kutupa miradi mingi ya maendeleo na inaendelea kutupatia hatuna budi kumshukuru kwahyo kufanya kwetu kazi na kusimamia vizuri kutafanya tuendele kupata miradi mingi zaidi na niwaombe tushirikiane”.