WATAALAMU WA AFYA WAPATIWA MAFUNZO YA MAADILI, SHERIA NA KANUNI ZA UTUMISHI WA UMMA
Jumla ya wataalamu 30 ambao ni madaktari,wauguzi,maafisa afya na wahudumu wa afya ambao ni waajiriwa wapya wamepatiwa mafunzo ya maadili kazini ambayo lengo lake ni kuwafundisha na kuwaelekeza namna ya kufanya kazi kwa kufuata maadili,sharia na kanuni za utumishi wa uuma.
Hayo yalisemwa na afisa utumishi wa halmashauri ya mji Bi.Paschalina Mabena na kusema ,”tumewaita hapa ili kuwakumbusha na kuwafundisha kwa kuwa ninyi ni waajiliwa wapya ili muweze kuepuka makosa ya kiutumishi hivyo niwaombe muepuke uchelewaji na utoro wa rejareja,lakini pia nidhamu kazini ikiwa ni pamoja na ushirikiano,kufanya kazi kwa kujituma pamoja na kuwa na maadili mema katika maeneo yetu ya kufanyia kazi”.
Kwa upande wake afisa wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa(TAKUKURU) Bw.Onesmo Mdegela amewasisitiza watumishi hao kufanya kazi kwa kufuata maadili ikiwa ni pamoja na kuepukana na vitendo vya rushwa ili kuweza kufanya kazi kwa ufanisi ikiwa ni pamoja na kuacha kupokea rushwa kwani baadhi ya watumishi wamekuwa wakipokea rushwa katika maeneo yao ya kazi.
Aidha Mdegela ameendelea kuwasisitiza kufanya kazi kwa kufuata kanuni na sharia za utumishi kwa kuanzia mavazi,mionekano kwa kufuata miongozo ya dini na miiko ya jamii na kusema”serikali inapotengeneza makatazo ya maadili ya utumishi wa umma yanafuata maadili hivyo tujitahidi kuyafuata na kuyatii ”.