Kaimu Afisa elimu msingi Halmashauri ya Mji Kasulu Michael Mahewa Yusuph awasisitiza wazazi ambao hawajaandikisha watoto wao madarasa ya awali na darasa la kwanza kuhakikisha wanafanya hivyo kabla muda kuisha.
Akizungumza na wazazi pamoja na waalimu alipokua katika ukaguzi wa zoezi la usajili wa wanafunzi mapema wiki hii Amesema wazazi ambao bado mpaka Sasa hawajapeleka watoto shule wakawaandikishe Mara moja hata kama hawana sare za shule mtoto aanze kusoma huku akieleza namna Halmashauri ilivyojipanga kupokea wanafunzi hao kwa kua na madarasa na walimu wa kutosha.
"Kwa mwaka huu Halmashauri inatarajia kupokea wanafunzi wa darasa la awali 7903, wasichana 3951 na wavulana 3952, ambapo mpaka sasa imepokea wanafunzi wa awali jumla 3651 wavulana 1791 na wasichana 1860 hivyo tumefikisha asilimia 56 kwa upande wa shule ya awali.
Aidha kwa upande wa msingi Halmashauri ina uwezo wa kupokea wanafunzi wa darasa la kwanza 7114 wavulana3470 wasichana 3644 ambapo mpaka Sasa jumla ya wanafunzi 4405, sawa na asilimia 61walioripoti huku wavulana wakiwa 2239 na wasichana 2166 katika shule zote za msingi zilizopo katika halmashauri ya mji Kasulu”
Pia ameongeza kuwa Halmashauri Ina madarasa ya nyongeza 45 yaliotokana na mradi wa boost ambapo serikali kuu kupitia Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ametoka fedha za kujenga madarasa hayo kwa mwaka 2023/23 ili kuhakikisha wanatatua changamoto ya miundombinu ya madarasa kwa shule za awali na shule za msingi.