Na Mwandishi Wetu
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa kasulu Dr.Peter Janga kwaniaba ya mkurugenzi wa Mji amezindua zoezi la utoaji wa chanjo Kwa halmashauri ya Mji wa kasulu ambalo zoezi hilo litadumu Kwamuda wa siku nne kuanzia 21 septemba na kumalizika 24 septemba Kwa kata zote 15.
Aidha Janga amewaasa wananchi kuwaruhusu watoto wao wenye umri wa kuanzia miaka 0 mpaka 8 kupata chanjo ya polio ambayo itawakinga na ugonjwa wa kupooza na kuelezwa kuwa zoezi hili litapita nyumba Kwa nyumba ,kwenye taasisi,masoko na stendi za mabasi na kuwasisitiza kuwa chanjo hii haina madhara na hivyo timu za uchanjaji ziwafuate walengwa majumbani na kuwawekea alama na si kuwakusanya watoto sehemu moja ambayo itasababisha kutokuweka alama katika nyumba ambazo watoto wamechanjwa.
Kwa upande wake Mratibu wa chanjo Halmashauri ya Mji Kasulu Bi Happyness Munis amesema,“malengo yetu katika zoezi ili la chanjo ya polio ni kuchanja watoto 86,760 naiomba jamii kutoa ushirikiano Kwa watoa huduma kwani zoezi hili ni muhimu Kwa kuwakinga watoto wetu dhidi ya ugonjwa wa polio ambao unaleta ulemavu wa kudumu au kifo na pia chanjo hizi zimethibitishwa na nisalama.
Naye Mratibu wa Elimu ya Afya Kwa Umma Be.Marcus Peter amesema kuwa wamefanya kazi ya uhamasishaji Kwa njia mbalimbali za ugawaji wa vipeperushi,rediona matangazo Kwa njia ya gari pia jamii imeonyesha mwitikio mkubwa WA zoezi hili japo kuna baadhi ya wananchi wamekuwa na Imani potofu kuwa chanjo hizi sio salama na hivyo kuwaomba kuondokana na dhana hizo na kuruhusu watoto wao wapate chanjo ya polio.
Baadhi ya wananchi ambao watoto wao wamepatiwa chanjo hiyo ya polio wamesema,“Kwanza tunafuraha Kwa watoto wetu kupata chanjo hii kwani tutakuwa tumewakinga na ugonjwa huu wa polio na Sisi tulokuwa na dhana za kuwa chanjo hizi sio salama lakini baada ya watoto wetu kupata chanjo bila madhara yoyote tutaenda kuwa mabalozi Kwa wenzetu na wao waruhusu watoto wao wapate chanjo ilinkuwakinha na ugonjwa wa kupooza ama kifo”.