HALMASHAURI YA MJI WA KASULU IMEPIMA VIWANJA KATIKA MJI MPYA WA KISASA ENEO LA MTUNDU KABANGA MKABALA NA SHULE YA SEKONDARI YA MUKA KWA AJILI YA MATUMIZI MBALIMBALI YAKIWEMO MAKAZI YA UJAZO WA JUU, KATI NA WA CHINI, BIASHARA, MASOKO, SHULE ZA MSINGI NA AWALI, ZAHANATI NA HUDUMA ZA KIDINI. VIWANJA HIVYO VIPO UMBALI WA KILOMITA TISA KUTOKA MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI YA MJI. MIUNDO MBINU KAMA UMEME, BARABARA PAMOJA NA MAJI KATIKA ENEO LA MRADI INAPATIKANA KWA URAHISI ZAIDI.